Moja
ya taarifa zilizochukua headline wiki iliyopita ni kuhusiana na tukio
la mtu mmoja kuruka ukuta wa ikulu ya Marekani, na baadaye kukamatwa
baada ya kushambuliwa na mbwa kabla ya kutiwa nguvuni na walinzi wa
ikulu hiyo, Secret Service.
Habari zinasema hii si mara ya kwanza
kwa Mnigeria Dominica Adesanya (23) kuruka ukuta wa White House, na
safari hii baada ya kumfikisha mahakamani imebainika kuwa ana tatizo la
akili hivyo hawezi kushitakiwa akiwa na hali hiyo.
Daily Mail
imeripoti kuwa baada ya
mahakama kuthibitisha vipimo kutoka hospitali
kuwa ana tatizo hilo, mahakama iliamuru awekwe chini ya ulinzi huku
akipata matibabu ya ugonjwa huo mpaka Desemba 22 kesi yake itakapotajwa
tena mahakamani hapo.
Adesanya ametolewa mahakamani hapo akipiga kelele za kuomba msaada huku akilaumu kitendo cha kukamatwa kwake.
Hii ni mara ya pili kwa jamaa huyo
kuruka ukuta wa White House, ambapo mara ya kwanza Adesanya ambaye ana
asili ya Nigeria kufanya hivyo ilikuwa Julai 27 majira ya saa 4 usiku
mwaka huu, na kurudia tena Oktoba 23 majira ya saa 1 jioni.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako