Mwana
Diplomasia kutoka Ghana ambaye pia ni Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa
Mataifa (UN) Kofi Annan amesema ugonjwa wa Ebola ni wa ‘maskini’ na sio
matajiri.
Annan amesema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na kituo cha CNN
ambapo amezungumzia sababu kadhaa zinazopelekea mapambano ya dhidi ya
Ebola kuchukua muda mrefu huku maelfu ya watu wakipoteza maisha.
Katibu Mkuu huyo mstaafu amesema Ebola
ni
ugonjwa wa maskini kwa kuwa tangu ugundulike ni takribani miaka 40
imepita, ambapo kwa nchi tajiri ingewezekana kufanyika tafiti ambazo
zingesaidia kupata ufumbuzi wa tiba ya ugonjwa huo, kitu ambacho nchi
maskini za Afrika hazina uwezo wa kuwekeza kwenye tafiti hizo.
Aidha, Annan ameonekana kuvunjwa moyo na
jitihada zinazofanywa na mataifa makubwa ikiwemo Marekani kutangaza
utaratibu mwisho wa wiki iliyopita wa kuwaweka karantini wauguzi na
madaktari waliotoka Afrika Magharibi kwa siku 21, kitu ambacho
kinarudisha nyuma ari ya wahudumu hao kujitolea kusaidia wagonjwa kwenye
nchi zilizoathirika na Ebola.
Amesema njia pekee ya kuimaliza Ebola ni
kufanya jitihada na mapambano ya pamoja katika kuzisaidia nchi za
Afrika Magharibi na sio kwingineko, na kuongeza kuwa Afrika inachohitaji
ni msaada wa vifaa, madawa na wauguzi ili kupambana na Ebola.
Mpaka sasa Liberia, Guinea na Sierra
Leone zimetajwa kuathiriwa zaidi na Ebola, huku takwimu zikionesha zaidi
ya watu 4,900 wamefariki na wngine zaidi ya 10,000 kupatwa na
maambukizi ya ugonjwa huo
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako