WAATHIRIKA
wa milipuko ya mabomu iliyotokea katika Ghala la Jeshi la Wananchi
Tanzania (JWTZ) Mbagala Aprili 29 mwaka 2009 wameibuka upya wakimuomba
Rais Jakaya Kikwete kuwasaidia wapate malipo stahiki kutokana na
milipuko hiyo iliyosababisha vifo na kuharibu nyumba na mali zao
mbalimbali.
Ombi
hilo limetolewa na waathirika hao kupitia Mwenyekiti wao Steven Gimonge
katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na waathirika hao zaidi ya 300
uliofanyika leo asubuhi viwanja vya Shule ya Msingi Mbagaala Kuu iliyopo
Manispaa ya Temeke.
Alisema
kwa muda mrefu waathirika hao wamekuwa wakiidai serikali iwalipe fidia
tangu uharibifu ulipotokea ambapo serikali ilikubali ingawa fidia
waliyolipwa awali haikulingana na uharibifu uliowapata.
Gimonge
alisema pamoja na fidia hiyo ndogo walipewa fursa ya kuandika barua za
mapunjo ambapo kwa mara kadhaa walilipwa fidia ndogo ambapo aslitolea
mfano mtu kulipwa fidia ya sh.1400, 2700, 1950 na 4900 mpaka Machi 12
mwaka jana kufikia uamuzi wa kupanga maandamano ya kwenda Ikulu kumuona
Rais Jakaya Kikwete.
Aliongeza
kuwa wanapenda kumkumbusha Rais Jakaya Kikwete kuwa alipokwenda
kuwafariji baada ya milipuko hiyo alitoa ahadi ya kuwapa kifuta machozi
pamoja na kufidiwa na hata kijiko kilicho potea lakini hadi leo hii
wamekuwa wakipigwa danadana.
Katika
hatua nyingine wamemlalamikia Mbunge wao Dk.Faustine Ndugulile kwa
kuwaacha bila ya kuwasaidia wakati alionesha njia ya kulipekea suala
hilo Bungeni lakini tangu afike huko amebadilika na hakuna mawasiliano
yoyote jambo ambalo linawashangaza.
Waahtirika
hao wanamuomba kwa mara nyingine Rais Kikwete awasaidia kupata fidia
hiyo kwani ile iliyotolewa awali ilikuwa kidogo ukilinganisha na ukubwa
wa kuathirika kwao.
Mwenyekiti
wa waathirika wa mabomu wa Mbagala Kuu, Steven Gimonge akionesha
daftari lenye majina ya waathirika hao na jinsi malipo yalivyofanyika
wakati akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi katika mkutano wa
hadhara uliowahusisha waathirika wa mabomu hayo yaliyolipuka katika
ghala la Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Aprili 29,2009.
Mwenyekiti
wa waathirika wa mabomu wa Mbagala Kuu, Steven Gimonge, akisisitiza
jambo katika mkutano huo. Kulia ni Katibu wa Waathirika hao, Thomas
Mbasha. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba
0712-727062)
Waathirika hao hapa wakionesha mabango yenye ujumbe tofauti tofauti.
Mmoja
wa waathirika wa mabomu hayo akiwa amejiinamia kwa huzuni huku
akitafakari kama Rais atawaonea kwa jicho la huruma wapate fedha hizo
kulingana na ukubwa wa kuathirika kwao.
Mabango zaidi yenye ujumbe tofauti yakioneshwa mbele za kamera za wanahabari.
Waathirika
hapo wakiwa kwenye mkutano huo kujadili jinsi serikali itakavyowapatia
fedha zao kulingana na ukubwa wa kuathirika kwao baada ya malipo ya
awali kudai walipunjwa.
Waathirika hao wakiwa kwenye mkutano huo uliofanyika Viwanja vya Shule ya Msingi ya Mbagala Kuu Dar es Salaam leo asubuhi.
Baadhi ya wazee na vijana waathiriwa wa mabomu hayo wakiwa kwenye mkutano huo.
Waathirika wakisisitiza kulipwa malipo hayo ya ziada baada ya awali kudaiwa kutolewa kidogo.
Mkazi wa Mbagala Kuu, Johanaina Mkukumbe akielezea jinsi walivyoa athiriwa na mabomu hayo pamoja na fidia kiduchu waliyolipwa.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako