Imetokea Mitaa ya Coco Beach DAR
Imetokea pande za COCO BEACH kuna
JAMAA bana aliiba NDINGA kwa BI MKUBWA wake akaenda nalo BEACH alipofika
kwa mbwembwe akamkabidhi DEMU wake aendeshe kumbe DEMU hajui KUNYONGA
bana si akalipandisha milimani kule kwa mwedo wa kasi akashindwa kufunga
breki akaliangusha toka juu mlimani mpaka chini kwenye yale maporomoko.
Kwa sasa DEMU yupo MUHIMBILI ICU
kaumia vibaga sana na mchizi nae kavunjika MKONO wa kushoto sa sijui
alikua anataka kulizuia NDINGA kwa mikono daaaah Mbwembwe hazifai.
Bi mkubwa alipovutiwa waya alifika
fasta eneo la tukio na alipoliona NDINGA lake lipo kwenye hali ya
UCHAPATICHAPATI aliangua kilio kama kafiwa na mumewe.
NB: Imewekwa kama ilivyotumwa.
CREDIT:GONGMIX
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako