Baba
mchungaji, ni nini hiyo? Ndivyo walivyosikika wakiuliza baadhi ya watu
waliokatiza kwa Mchungaji Michael Semeni wa Kanisa la Living Word
Ministry lililopo Ukonga- Majumba Sita jijini Dar es Salaam.
Mkasa
mzima ulijiri Julai 3, 2014 ndani ya ofisi za mchungaji huyo huku
mlalamikaji mkuu akiwa na mwanaume aliyedaiwa kuwa ni mume wa mwanamke
aliyekutwa na Semeni.
Sekeseke
hilo lilitokana na madai kwamba, Mchungaji Semeni alinaswa akiwa na
mwanamke huyo aitwaye Erizabert Kisanda, mkazi wa jijini Mwanza ambaye
alifika Dar kuonana naye kwa ajili ya kumwombea maombi maalum ya kiroho
‘deliverance’ kutokana na matatizo ya mke huyo kushika mimba na kutoka
kila wakati.
...Mara baada ya fumanizi.
OFM KAMA KAWAIDA YAKE
Siku
ya tukio, makamanda wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) walikuwa mitaani
katika viunga mbalimbali vya Jiji la Dar wakisaka matukio, ndipo
walipojikuta wakitokea eneo lenye kimbembe.Baadhi ya watu waliozungumza
na Ijumaa Wikienda walidai kuwa mchungaji huyo alinaswa na mke huyo wa
mtu hivyo kuzua tafrani kati yake na mwanaume anayedaiwa ni mumewe.
Mchungaji akihojiwa na kamanda aliyeshirikiana na OFM katika operesheni hiyo ya kufichua uovu kanisani hapo.
MTU WA KARIBU
Akizungumza na gezeti katika eneo la tukio, mtu mmoja aliyedai ni ndugu wa mwanamke huyo alisema:
“Iko
hivi! Huyu mwanamke alikuja Dar kwa mchungaji kwa lengo la kuombewa
apate mtoto. Alikuwa na tatizo la uzazi kwani kila alipopata ujauzito,
akikaribia kujifungua tu mimba inaharibika.
“Kutokana
na tatizo hilo, ndipo akashauriwa akamwone mchungaji huyo ndipo
akafunga safari kwenda kumuona na kumweleza tatizo lake, mchungaji
akamwambia ni tatizo dogo sana kwake.”
AHADI YAPANGWA
Ilizidi kudaiwa na ndugu huyo kwamba, ahadi ilipangwa ambapo mwanamke huyo alitakiwa kurudi siku hiyo ya tukio.
Mchungaji akichukuliwa kwenda polisi.
MAOMBI YALIVYOKUWA
Mambo
yaliendelea kuhabarisha kwamba, siku ya tukio, mwanamke huyo alifika
kuombewa ambapo mchungaji huyo alizama kiroho zaidi kwa muda wa saa
mbili, yaani dakika mia na ishirini.
“Baada
ya kumaliza maombi hayo ndani ya kanisa ndipo mchungaji huyo
akamchombeza kwa kumwambia wazame chumbani akamwombee zaidi,” chanzo
kilisema.
AKUTWA NA PENSI!
Wapashaji
wa mkasa huu wanadai kuwa wakiwa chumbani sasa, mke hana nguo,
mchungaji akiwa ndani ya kipensi tu, mwanaume aliyedaiwa ni mume na dada
yake walitokea kusikojulikana na kuwavaa.
Huu ni mwonekano wa ndani wa kanisa la Living Word Ministry lililopo Ukonga, Majumba Sita jijini Dar es Salaam.
NENO SAMAHANI
Baada
ya kunaswa, mchungaji huyo alirudiwa na fahamu na kuanza kuomba
asamehewe huku akimlaumu shetani kwamba alimpitia naye akapitika kweli.
“Duh! Yamenikuta jamani, naomba mnisamehe ni shetani tu alinipitia,” alisikika akisema mchungaji huyo.
MUME ALIJUA?
Swali kubwa lililotawala eneo la tukio ni kuibuka kwa mwanaume huyo, kwamba alijua mkewe anakwenda kwa mchungaji huyo?
Baadhi
ya watu walisikika wakisema kuwa wana wasiwasi kwamba, mwanaume huyo,
mkewe na mawifi walijua litakalokwenda kutokea kwa mtumishi huyo wa
Mungu hivyo walimtega naye akauingia mtego huo!
Bango linaloonyenesha ratiba za ibada zinazofanyika kanisani hapo.
ALICHOMWA?
Maneno
ya watu ni mengi sana, mawifi nao walisikika wakimsakama mchungaji kwa
kudai kuwa alizoea kuchezea wengine lakini si kwa wifi yao huyo bila
kufafanua maana ya madai yao hayo hivyo kujenga dhana kwamba huenda kuna
watu walimchoma mchungaji huyo kwa mume wa mwanamke huyo.
NI KWELI MIMBA HUHARIBIKA?
Baada
ya kumalizika kwa tafrani hiyo, OFM walipenda kujua kama madai ya
mwanamke huyo kuharibu mimba kila anapokaribia kujifungua ni ya kweli,
wifi mmoja alithibitisha ni kweli na kwamba, mwanamke huyo ameshazunguka
sana kutafuta dawa ya kuondoa tatizo hilo lakini wapi!
MALALAMIKO KUHUSU MAOMBI YA DELIVERANCE
Kumekuwa
na malalamiko kadhaa kutoka kwa baadhi ya waumini wa Kikristo nchini
wakilalamikia maombi ya deliverance yanayofanywa na baadhi ya
wachungaji, wengine wakisemekana kutumia nafasi hiyo kuzini na wake za
watu.
Maombi
hayo yanayofanywa na baadhi ya watumishi wa Mungu, hupewa kipaumbele
cha muombewa na mwombaji kuwa wawili tu, wakati mwingine hufanyika nje
ya kanisa kama hotelini au gesti!
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako