Watu watatu wakazi wa Mwananyamala Jijini Dar Es Salaam wamejeruhiwa katika tukio lililohusisha risasi za moto linalodaiwa kufanywa na polisi baada ya kukutwa wakikesha kwenye ngoma maarufu za Kigodoro, ambazo tayari zimekwishapigwa marufuku na jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam.
Tukio hilo lilitokea majira ya saa kumi na nusu jioni katika eneo la shule ya msingi kisiwani ambapo mmoja wa majeruhi hao tayari amekwisahruhusiwa kurudi nyumbani na mwingine
akiendelea na matibabu kwenye hospitali ya Mwananyamala.
Wakiwa kwenye ngoma hiyo maarufu Jijini Dar es Salaam ya Kigodoro, eneo
la Kisiwani mwananyamala, mara gahfala polisi walivamia eneo hilo, na
kusimamisha shughuli nzima kwa madai ya kucheza wakiwa hawana nguo,
jambo ambalo ni kinyume na maadili.
Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa kipolisi Kinondoni Kamishna msaidizi Camillius Wambura anathibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa kipolisi Kinondoni Kamishna msaidizi Camillius Wambura anathibitisha kutokea kwa tukio hilo.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako