Baada ya ukame wa tuzo hatimaye mwaka huu alichukua tuzo ya
mwana HipHop bora katika tuzo za KTMA na akafanikiwa kua moja kati ya wasanii wachache walioshinda tuzo mwaka huu kuchaguliwa kujiunga na Kill Tour ambayo itazunguka miko mbalimbali hapa Bongo.
Jumamosi iliyoisha ilikua zamu
ya wakazi wa Mwanza kupata shangwe za Kill Tour na baadhi ya wasanii
waliodondosha show ya nguvu ni Vanessa Mdee, Weusi, Ben Pol na Fid
mwenyewe. Wasanii wengine wote walipiga show vizuri tatizo lilikuja pale
alipopanda Fid jukwaani.Burudani aliyotoa sio ile wakazi wa Mwanza
waliyotarajia inadaiwa kua Fid Q alikua amelewa sana. Kwa mujibu wa
chanzo chetu kilichokua backstage kilisema kua kulikua na bia za bure
zilizokua zikitolewa kwa wasanii na kampuni ya bia ya Kilimanjaro ndizo
zilidaiwa kua chanzo cha Fid kuharibu stejini.
Chanzo hicho kiliendelea kusema kua pamoja na kutoa burudani mbaya
lakini alikua akiyumba yumba na kutaka kudondoka. Mwisho wa siku
alishuka lakini watu walibaki wakilalamika. Mashabiki wake hawakuridhika
wakamfata Insta na kulalamika na haya ni baadhi ya maoni
salumusaid broo mi nakukubal san ila jan sijafurahia shoo ata kidogo
erickhenry773 Ukaamua kuwa ahmada jana underperfomance kichz
Baada ya kuona watu wamemind sana Fid Q aliamua kufunguka na kusema haya kuhusu kufanya kwake vibaya ”Afya ilileta mgogoro.. Nxt time kama vp.. Pole kwa usumbufu uliojitokeza ��”
Baada ya kuona watu wamemind sana Fid Q aliamua kufunguka na kusema haya kuhusu kufanya kwake vibaya ”Afya ilileta mgogoro.. Nxt time kama vp.. Pole kwa usumbufu uliojitokeza ��”
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO