BASI MPYA ZA NDENJELA JET ZITAKAZOANZA SAFARI MWEZI WA 8 |
Ndenjela Luxury Coach ni kampuni ya kisasa kabisa ya usafiri wa abiria
kati ya jiji la Da r es salaam na jiji la Mbeya na pia kutoka jiji la
Mbeya kwenda kwenye mji wa Sumbawanga kwa safari za kila siku. Hii ni
kampuni ilikuja kuleta ushindani kwenye nyanja ya usafiri wa abiria hapa
nchini kwani ni moja ya kampuni inayotoa huduma bora kabisa kwa abiria
wake kama Huduma ya kwanza kwa mtu anayejisikia vibaya ama kupatwa na
ugonjwa akiwa safarini, huduma ya vinywaji, vitafunwa abiria wawapo
safarini bila ya kusahau uhifadhi mzuri wa mizigo ya abiria.
Uwapo ndani ya mabasi ya kampuni hii utapata kufurahia huduma ya Video
za aina mbalimbali na za kusisimua kutoka kwenye luninga zilizo kila
pembe ya basi hilo kama uonavyo pichani. Kwasasa kampuni hii imejipanga
kuingiza barabarani basi mpya luxury na za kisasa kama uzionavyo pichani
ambazo zitaanza safari mnamo mwezi wa 8 mwaka huu kwa safari za kila
siku kutoka Dar kwenda Mbeya na pia kutoka Mbeya kwenda Sumbawanga.
Kuondoka Dar ni saa: 12:30 Asubuhi kwenda Mbeya na pia muda huohuo kutoka Mbeya kwenda Dar,
Mbeya kwenda Sumbawanga basi linaondoka saa 12:45 asubuhi na pia saa tano asubuhi,
Sumbawanga kwenda Mbeya basi linaondoka saa 1:30 asubuhi na pia saa 7:30 mchana.
Kumbuka safari hizi ni za kila siku, kufanya booking ya safari yako piga simu namba
0718 600042 - Dar es salaam,
0718 600043 - mbeya,
0687 600045 Sumbawanga.
Karibuni.
MUONEKANO WAKE KWA NYUMA |
UZURI WA BASI HILO KWA NDANI LIKIWA NA TV KILA KONA |
MOJA YA BASI HIZO AINA YA ZHONGTONG LINAVYOONEKANA KWA MBELE |
NDENJELA JET |
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako