Love is blind lakini wanaopenda wana macho. Hapa
inajidhihirisha kwa Chuchu hans, baada ya kuzunguka sana mwisho wa siku
kufika alipotaka. Mwanadada huyo alikuwa Miss Tanga 2010 na kuingia
bongo movie yuko ndani ya mapenzi mazito sana na legend wa bongo movie
Raymond Kigosi a.k.a Ray , ceo wa RJ company.
Katika kuonyesha how deep her love kwa kijana huyo Chuchu aliamua
kujichora tatoo yenye jina na Star huyo na kwa sasa Ray ameshahama kwao
na kuhamia sehemu nyingine kuishi na binti huyo wa kitanga mwenye
muonekano wa point five yani chotara flani na kwa sasa wawili hao
wanaishi pamoja. So kama kuna anaesubiri waachane leo au kesho basi
wawili hawa bado wapo sana na hata ndoa haitakuwa mbali sana kwani vibe
ilipombana mdada huyo alijikanjaga na kuropoka kwamba target yao ni
kuoana ila hajajua itakuwa lini lakini lazima ndoa itakuwepo , basi
tuwatakie kila la kheri wawili hawa…