Wamenaswa: Mashabiki wawili waliojipaka rangi nyeusi wakiwa katika pozi kwenye mchezo baina ya Ujerumani na Ghana.
SHIRIKISHO la soka Duniani, FIFA
linachunguza picha zilizozagaa zikiwaonesha mashabiki wakiwa wamejipaka
rangi nyeusi katika mchezo wa kundi G baina ya Ujerumani na Ghana.
Picha zilizochapishwa kwenye
mitandao ya kijamii zinaonesha wanaume wawili, wanaoonekana kuwa
mashabiki wa Ujerumani, wakiwa na sura nyeusi kwenye uwanja wa Fortaleza
jumamosi iliyopita.
FIFA imesema kamati yake ya maadili ipo katika majadiliano ya kufungua kesi.
Chini ya uchunguzi: FIFA inachunguza ripoti zinazoeleza kuwa mashabiki wa Ujerumani walijipaka rangi nyeusi.
Wanatazama mechi: Mashabiki wawili walinaswa na kamera katika sare ya 2-2 baina ya Ujerumani dhidi ya Ghana.
“Siku zote tunachukua ushahidi
wote na kuupeleka kamati ya maadili. Ni kamati ya maadili
itakayokutana,” Msemaji wa FIFA amewaambia The Guardian. “Kama
kutaonekana kuna ukweli kesi itafunguliwa. Hilo lipo juu ya kamati ya
maadili, wao ndio watachukua maamuzi”.
FIFA huwa wanayawajibisha mashirikisho ambayo mashabiki wake wanaonesha utovu wa nidhamu uwanjani.
Katika tukio la pili, mtu aliingia uwanjani kipindi cha pili wakati wa sare ya 2-2.
Mtu huyo ambaye hakuwa na shati aliripotiwa kuwa ni Mpoland na alijiandika namba za simu na anwani ya barua pepe tumboni kwake.
Kiungo wa zamani wa Portsmouth na
Sunderland, Sully Muntari, ambaye kwasasa anacheza AC Milan alimsalimia
mtu huyo kabla ya kuondolewa na maaskari wa usalama.
Msemaji wa kamati ya maandilizi
ya Brazil, Saint-Clair Milesi alisema mtu huyo aliingia kutokana na
uzembe wa mamlaka zinazohusika na usalama uwanjani.
Shabiki aliingia uwanjani katika sare ya 2-2 baina ya Ujerumani na Ghana.
credit: shafiidauda web
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako