| All Star Club Elizabeth New Jersey Diamond akikamua licha ya show kuchelewa
kuanza na wapenzi wa Diamond kushikwa na jazba wakitaka aendelee lakini
ikashindika kutokana na muda wa kufunga club kufika. wavuti.com imeshirikishwa picha hizi zote na Luke Joe/Vijimambo Blog |
AJ nae akifanya yake baada ya kupewa nafasi ya ufunguzi katika show hiyo iliyofanyika New Jersey.
AJ Ubao na Dirty Hary wakishambulia jukwaa kwenye show ya kufubgua pazia
iliyoanyika New Jersey na baadae Prezidaa wa Wasafi, Diamond Platnumz
kuwapagawisha mashabiki wake wa ukanda wa pwani ya mashariki.
Ni Rais wa Wasafi akishambulia jukwaa akiwa na madancer wake kwenye show
ya kukata na shoka iliyofanyika New Jersey na kuvuta mashabiki kutoka
kila kona ya pwani ya mashariki ambayo ni DC, PA, NJ, NY, CT, MA na
kwingineko
Diamond mwanamuziki wa kizazi kipya anayekimbiza vibaya mno kwenye anga
za Bongo Flava akipagawisha mashabiki wake New Jersey nchini Marekani.
Diamond na madancer wake wakijaribu kukata kiu ya mashabiki wake wa pwani ya mashariki.
Shabiki akidata na show ya pezidaa wa wasafi.
Shabiki akidatishwa na moja ya wimbo wa Diamond na kushindwa kujizuia kupanda jukwaani.
Mashabiki wa Diamond wakipagawa huku wengine wakipata taswira za hapa na pale.