Wakazi wa Iringa wameifunga awamu ya kwanza ya Kilimanjaro Music Tour wakiwa wamefurika katika Uwanja wa Samora kushuhudia wakali wa muziki nchini wakitoa burudani bila kujali hali ya hewa ya baridi.
Wakali wa Muziki akiwemo Snura, Linex, AY, Mwana FA, Profesa Jay, Izzo Bizness, Joh Makini, Juma Nature, Mwasiti, Nikki wa
Pili na Gnako Warawara walilishambulia jukwaa kwa takribani saa sita mfululizo na kukonga nyoyo za maelfu waliojitokeza kushuhudia Tamasha hilo.
Ziara hiyo iliyozunguka mikoa mitano
inatarajiwa kuendelea mwezi Agosti ikiwa ni kuupisha mwezi mtukufu wa
Ramadhani na inatarajiwa kwenda mikoa ya Mbeya, Kigoma, Mtwara, Dodoma
na kukamilishiwa Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako