A

A

PAMOJA NA YOTE, SUAREZ APOKEWA KISHUJAA URUGUAY, RAIS WA NCHI ALIKUWEPO PIA ...UMATI WA WATU NA MABANGO YA 'KUIDISI' FIFA


Na  Bin zubery
 MASHABIKI wa Luis Suarez walijitokeza kwa wingi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Carrasco jirani na Montevideo kumlaki mshambuliaji huyo aliyefungiwa Kombe la Dunia akirejea nchini Uruguay.
Akiwa amefungiwa mechi tisa za kimataifa na miezi minne kwa ujumla kujihusisha na soka, Suarez alirejea Uruguay akiiacha timu yake imetinga Hatua ya 16 Bora ya Kombe la Dunia.
Mashabiki walijimwaga mitaani hadi Uwanja wa Ndege kwenda kumpokea mshambuliaji huyo wa Liverpool nchini Uruguay, huku wengine wakiwa wamevaa picha yake kumtukuza nyota huyo.
Rais wa Uruguay, Jose Mujica alikuwas Uwanja wa Ndege pia kumpokea, lakini akaamua kuondoka katakana na ndege iliyokuwa inamrejesha Suarez kuchelewa. 

Mapokezi ya shujaa mhalifu: Mashabiki wa Luis Suarez wakiwa tayari kumpokea kipenzi chao akirejea Uruguay
Partisan: Supporters wanted to see the star striker arrive back in Uruguay following his ban
Partisan: Supporters wanted to see the star striker arrive back in Uruguay following his ban
Backlash: A supporter holds up a message aimed at FIFA after the ban given to Suarez
Shabiki akiwa ameshika bango la kuikandia FIFA kwa kumfungia Suarez
Fangs: A young supporter with some fake teeth in his mouth at Carrasco International Airport
Shabiki mdogo akiwa na meno bandia mdomoni mwake Uwanja wa Ndege wa Carrasco
Carnival: Spectators gather at the airport ready to greet the Liverpool striker
Watu wakiwa wamejipanga barabarani tayari kumpokea mshambuliaji huyo wa Liverpool
Rammed: The streets leading to Carrasco International Airport are crowded with fans waiting for Suarez
Barabara ya kuelekea Uwanja wa Ndege Carrasco watu wako tayari kwa mapokezi ya Suarez

Kwa sababu ya kuchelewa, umati wa watu wapatao 1,000 uliondolewa eneo la Uwanja wa Ndege na kuhamishiwa katika eneo la jeshi kuendelea kumsubiri Suarez awasili.
Mapema Suarez alipigwas picha akiwa na wachezaji wenake mjini Rio wakati wanawasili hotelini.
Uruguay itamenyana na Colombia katika 16 Bora ya Kombe la Dunia mechi ya timu za Amerika Kusini tupu.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako