JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Wasailiwa
1,281 kati ya 6,115 waliofanya usaili wa kwanza tarehe 13 Juni, 2014
jijini Dar es Salam kuomba nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji
(Assistant Inspector of Immigration) wanatarajiwa kuingia duru ya pili
na ya mwisho ya usaili huo baada ya kufanikiwa kufaulu usaili wa kwanza.
Usaili
huu ambao utafanyika kwa awamu utaanza tarehe 23 Juni hadi 03 Julai,
2014 na utafanyikia katika Bwalo la Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar
es Salaam kuanzia saa 1.30 asubuhi.
Tofauti
na usaili wa kwanza ambao ulikuwa wa kuandika na ulihusisha maswali ya
hesabu na ufahamu wa jumla, usaili wa awamu ya pili utakuwa wa maswali
ya ana kwa ana ambao utahusisha kupima uwezo wa msailiwa kujieleza na
kufafanua mambo.
Kuchaguliwa
kwa wasailiwa hawa kulifanyika baada ya kusahihisha majibu yao na
majina kuingizwa katika mfumo wa kimtandao ambao ulisaidia kuchagua
wasailiwa waliopata alama hamsini na kuendelea.
Majina ya wasailiwa hawa yanapatikana katika Tovuti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, www.moha.go.tz na ya Idara ya Uhamiaji, www.uhamiaji.go.tz na watatakiwa kuja na vyeti vyao halisi vya kuzaliwa, vya shule na picha mbili za pasipoti.
BOFYA LINK HIYO HAPO CHINI KUSOMA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI
http://www.moha.go.tz/phocadownload/Kuitwa%20Kwenye%20Usaili_Uhamiaji.pdf
http://www.moha.go.tz/phocadownload/Kuitwa%20Kwenye%20Usaili_Uhamiaji.pdf
Awali, kiasi cha wasailiwa 10,801 waliitwa kwa ajili ya usaili wa kwanza
baada ya kupokea maombi yao, lakini waliohudhuria ni 6,115 na kati yao
ndio walipatikana 1,281 ambao watasailiwa ili kupata watakaojaza nafasi
sabini (70) za Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji katika Idara ya Uhamiaji.
Sgn Isaac J. Nantanga
0754 484286
MSEMAJI,
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako