Rafiki
yangu ambae ni mwandishi wa habari wa Arusha255 amenipa ripoti fupi
kwamba majambazi waliingia kwenye duka moja la kubadilishia fedha Clock
tower karibu na house of wine Arusha mjini ambapo kifo cha huyu ndugu
kilitokana na yeye kupiga kelele baada ya kuona majambazi hao wakitenda
uhalifu.
Japo nasubiria ripoti kamili ya Polisi leo, taarifa za
mwanzo
zinasema Marehemu alipiga kelele hizo muda mfupi tu baada ya kutoka
kanisani na akawa anasubiri watoto wake kwenye eneo la tukio ila
alipoona dada ndani ya duka kavamiwa ndio akaanza kupiga kelele za
kuomba msaada.