MASTAA wa kike wanaotingisha Bongo,
Elizabeth Michael ‘ Lulu’ ( pichani) na Husna
Maulid, ilibaki kidogo wazichape
Kabla ya tukio hilo, awali wawili hao
waliwahi
kuingia kwenye bifu baada ya kudaiwa
walikuwa wanamgombea pedeshee mmoja
wa mjini, kila mmoja akijipa uhalali wa
kumilikiwa.Tukio hilo bichi kabisa lilitokea Juni 16, mwaka huu , Mikocheni jijini Dar es Salaam ambapo chanzo kinasema , wadada hao walikuwa wakirekodi sinema ambayo haijajulikana jina lake . “Ni kweli walikuwa wakirekodi filamu , lakini kuna muda walizinguana ila watu wanasema bado wanakasirikiana kutokana na ile ishu ya kunyang’ anyana mwanaume . “Joti ( Lucas Mhuvile – yule komediani wa Kundi la Orijino Komedi ) alikuwepo eneo la tukio na ndiye aliyewapatanisha, ” kilipasha chanzo hicho. Joti alipotakiwa kuzungumzia ishu hiyo , alikiri kutokea lakini kwenye kurekodi filamu huku akikataa kufafanua.
“We’ jua kuwa ilikuwa filamu , si ugomvi serious,” alisema Joti . Lulu hakupatikana kuzungumzia ishu hiyo lakini Husna alipopatikana alisema : “Tulitofautiana kikawaida tu kama wanawake lakini hatukufika kwenye mambo ya kupigana. ”
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako