Filipo Inzaghi ateuliwa kocha mpya wa AC Milan
AC Milan imemfuta kazi mkufunzi
wake Clarence Seedof baada ya kuhudumu kwa chini ya miezi 5 na
kumtangaza Filipo Inzaghi kama kocha mpya.
Seedof mwenye umri wa miaka 38 alikuwa amechukua
nafasiyake Massimiliano Allegri mwezi Januari, wakati timu hiyo ilikuwa katika nafasi ya 11 katika ligi kuu ya Italia Serie A na alama 30 nyuma ya viongozi wa wakati huo Juventus, ambao walishinda taji hilo mwisho wa msimu.
Filipo Inzaghi ameteuliwa kocha mpya wa AC Milan na kuchukua pahala pa Clarence Seedof