Mjumbe
wa Baraza Kuu Chadema ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya
Temeke Joseph Yona (kushoto) akiongoza wenzake kuingia Ofisi ya Msajili
wa Vyama leo kuwashitaki viongozi wa ngazi ya juu wa chama hicho kwa
kudaiwa kutotekeleza Demokrasia na kufuata Katiba ndani ya Chama.
Wanachama
na Viongozi wa Chadema wakiwemo wa Baraza Kuu la chama hicho, wakipiga
kwata kuelekea Ofisi za Msajili wa Vyama vya Siasa, jijini Dar es
Salaam, leo, kupeleka barua ya kumuomba Msajili huyo wa vyama, kuwataka
viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema kuzingatia Katiba ikiwemo kuitisha
kikao cha Baraza Kuu na kuzingatia matumizi bora ya fedha za Chama.
Yona
akisaini kitabu cha wageni kwenye kwenye mapokezi ya Ofisi ya Msajili
wa Vyama Jijini Dar es Salaam, alipowasili ya ujumbe wake. Kulia kwa
Yona ni Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Kaliua mkoani Tabora ambaye ni
Mjumbe wa Baraza Kuu na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Chadema, Jorum Mbogo
Naibu Msajili wa vyama vya Siasa Nchini akimkaribisha Yona na msafara wake.
Wanachama
waliofuatana na wajumbe wa Baraza Kuu Chadema wakisubiri kuwasisha
barua yao kwa Mkuu wa Masijala wa Ofisi ya Msajili wa vyama.
Yona akionyesha abarua ambayo baadaye aliikabidhi masijala kwa ajili ya kumfikia Msajili wa vyama
Yona akikabidhi barua yao, kwa Mtunza kumbukumbu Mkuu wa Ofisi ya Msajili wa vyama, Jihadhari Saidi.
Yona akizungumza nje ya Ofisi ya Msajili baada ya kuacha barua yao kwa Msajili wa Vyama
Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Kaliua mkoani Tabora ambaye ni Mjumbe
wa Baraza Kuu na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Chadema, Jorum Mbogo akisoma
taarifa yao kabla ya kwenda kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
baadaya ya kutoka kwa Msajili ya vyama.
Baadhi ya wanachama wanaodaiwa kuwa wa Chadema wakiwa na mabango nje ya Ofisi ya Msajili wa vyama
Eti Bora Chadema ife kuliko Mbowe kutapeli?
Chadema wakiomba msaada kwa Msajili wa vyama
Ujumbe mzito kwa Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe
Wanachama na Viongozi wa Chadema wakiwemo wa Baraza Kuu la chama
hicho, wakiwa nje ya Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali leo
kupeleka maombi ya kutaka Mkaguzi huyo wa Hesabu za serikali kufanya
ukaguzi wa hesabu wa Chadema kwa madai kwamba viongozi wa ngazi za juu
wanazitafuna.KWA HISANI KUBWA YA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako