
Mbovumbovu za staa! Staa wa sinema za
Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe anadaiwa kuwa tilalila na kujikuta
akipiga mwereka kwenye shughuli ya kibao kata cha mwigizaji mwenzake,
Vanita Omary.
Kwa mujibu wa ‘shushushu’ wetu aliyekuwa
ndani ya nyumba, tukio hilo lilijiri kwenye Ukumbi wa PG Hall (zamani
FM Club), Kinondoni jijini Dar ambapo mastaa kibao walihudhuria.
Ndani ya kibao kata hicho, Wolper alicharuka kipombepombe kwa kucheza ovyo na kukimbiakimbia akiwa tilalila.
Katika kukimbia huko, ndipo akapiga mwereka na kuanguka huku akijaribu kusimama kwa kuchechemea.
Baadhi ya wageni waalikwa walibaki wakimshangaa na kusema kuwa hapendezi akinywa pombe kwani ustaarabu wote unapotea.
Baadhi ya wageni waalikwa walibaki wakimshangaa na kusema kuwa hapendezi akinywa pombe kwani ustaarabu wote unapotea.
Mbali na pombe pia alikuwa kivutio kwa
staili ya ukataji wake wa mauno akiwa na kivazi kilichoacha nje mapaja
yake akiwa na rafiki yake aliyetajwa kwa jina moja la Vivi.
Katika hatua nyingine, Vanita alijikuta
akiangua kilio baada ya wapiga ngoma wa kibao kata ‘kuwa feki’ na
kushindwa kufanya kazi kama walivyoahidi.
Kutokana na hilo, baadhi ya mastaa kama
Aunt Ezekiel na Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ waligoma kucheza na kukizomea
kibao kata hicho ambacho kililetwa na MC (jina linahifadhiwa) akidai
kuwa amewatoa Bagamoyo na wana ufundi wa hali ya juu.