Katika
hali isiyokuwa ya kawaida na ya kushtukiza wasanii Wema Sepetu na Mtitu
usiku wa kuamkia jumatatu walizinguana kinoma kaisi cha kutaka kutoana
roho kwa kile kinachodaiwa Wema kujibu nyodo mara baada ya kupata
taarifa za msiba wa Adam Kuambiana.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu kilichokuwepo eneo la tuki kilisema kuwa chanzo
cha ugomvi huo ni baada ya kifo cha Adamu wasanii wote walifika kwa
wakati eneo la msiba isipokuwa Wema Sepetu ambae hakuonekana mapema.
Hata
hivyo baada ya kutoonekana Wema msibani mwenyekiti wa Bongo Movie
alimpigia simu Wema na kumueleza kama ameusikia msiba wa Adamu"
Unaambiwa Wema alimjibu kunya steve kiasi cha kukata simu, kwani
alimwambia kama ndiyo ameusikia msiba kwa hiyo steve anatakaje?"
Kilisema chacho hicho
Hata
hivyo Wema inadaiwa aliendelea kusema kama Adamu amekufa si siku zake
zilikuwa zimefika, ndipo steve alipomwambia anatakiwa aonekane msibani
kwani wasanii wenzake wote wapo yeye tu ndo haonekani, ndipo Wema
alipojibu kuwa mbona yeye alipofiwa na babaake hakumuona Adamu kwa hiyo
asilazimishwe kama ataenda basi kwa hiari yake.
Hata hivyo tulimtafuta Wema kupitia simu yake ya kiganjani ili kuelezea tukio hilo lakini hakuweza kupatikana.
Hata
hivyo siku ya Jumatatu usiku wakati wa mkesha ndipo Wema alipoonekana
akiwa na Aunt Ezekiel ambapo mtitu ambae alikuwa tilalila huko msibani
Bunju na alipomuona Wema akaanza kumtusi ya nguoni ndipo wakaanza
kujibizana kiasi cha kukunjana huku akimpaka juu ya majibu aliyoyatoa
kwa mwenyekiti huyo wa bongo movie
.
Hata hivyo hadi chanzo cha chetu kinaondoka eneo la tukio kiliacha mtiti huo ukiendelea.
source: xdeejayz