A

A

Top 3 Videoz za Comrade Mwigulu Nchemba Zilizowafanya Upinzani Waonekane Watupu, na Upinzani Hawata Zisahau

Kutokana na Kukua kwa Kasi Kisiasa kwa Mwanasiasa Kinda Mh:Mwigulu Nchemba hapa Nchini kupitia Chama cha Mapinduzi,Licha ya Kuwa Mwanasiasa anayevuta tension kwa Mwananchi yeyeote anaposikia anazungumza ama Bungeni au sehemu yoyote ile Jukwaani au Kwenye Vyombo vya Habari kwa namna anavyojenga hoja zake kwa Mlengo wa Utaifa,Maslahi kwa Wananchi na Uzalendo wa hali ya Juu,Hii leo nimeguswa angalau Kukupa nafasi ya Kuangalia angalau Video tatu ambazo Katika Michango yake ndani ya Bunge Zimekuwa Gumzo sana. 

Video Na.1"Achanachana Bajeti ya Upinzani Bungeni"
Hii ni Video ambayo Mh:Mwigulu Nchemba aliweka Historia kwa Mara ya kwanza ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akichangia Bajeti ya Nchi Mwaka 2012/2013.Hii Video inatajwa kuwa ndio Iliweka Gumzo kwa Wanasiasa Nchini hasa Upinzani.Inasemekana Upinzani walianza hapa Kutambua Moto wa Mwigulu Nchemba kwenye Siasa.
VIDEO 2:
"Ahojia Uandishi wa Tarakimu kwenye Bajeti ya Upinzani"
Kwenye Video hii Mh:Mwigulu Nchemba anahoji Mapungufu Makubwa ya Uandishi wa
tarakimu kwenye Bajeti ya Upinzani,Hususani Kushinda kuandika Bilioni kwa tarakimu.

VIDEO:  3.
"Akichangia Bunge la Katiba 2014.Ahoji Mbowe na Jusa Kutaka Kupitisha Swala la Ushoga KimyaKimya"?.
Kwa mara ya kwanza akichangia Kweneye Bunge Maalumu la Katiba Mwaka 2014,Mh:Mwigulu Nchemba aamua kuweka wazi kuwa Kufanya mambo kwa Siri kuna watu wanataka Kupitisha Mambo Mabaya kwa Taifa Kimya kimya likiwamo Ushoga.>Angalia Video.
Video Zipo Nyingi alizochangia Bungeni,Lakini hizi ni baadhi tu zilizotikisa Nchini na Uga wa Siasa.
Na.Mtanzania Mzalendo.