
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote katika uwanja wa ndege wa kiwanda chake cha saruji cha Dangote Cement
Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos
alipotembela Mei 9, 2014. Kushoto ni Balozi wa Nigeria nchini Tanzania
Mhe. Dkt. Ishaya Samaila Majanbu

Rais Dkt Jakaya Mrisho kikwete akipata maelezo toka kwa mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote wakati akizungushwa kuangalia kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela Mei 9, 2014

Rais Dkt Jakaya Mrisho kikwete akipata maelezo toka kwa mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote wakati akizungushwa kuangalia kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela Mei 9, 2014

Rais Dkt Jakaya Mrisho kikwete akipata maelezo toka kwa mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote wakati akizungushwa kuangalia kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela Mei , 2014

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa kwenye machimbo ya kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela Mei 9, 2014

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa kwenye mtambo wa kuzalisha umeme wa kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela Mei 9, 2014

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa na mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote kujionea maeneo mbalimbali ya kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela Mei 9, 2014.

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa na mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote kujionea maeneo mbalimbali ya kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela Mei 9, 2014.

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa na mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote kujionea maeneo mbalimbali ya kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela Mei , 2014.

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa aina ya mali ghafi inayotumika alipotembelea kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela Mei 9, 2014

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa aina ya mali ghafi inayotumika alipotembelea kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela Mei 9, 2014
![]() |
| Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika mfuko wa saruji alipotembelea kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela Mei 9, 2014 |
- Ni kile kinachomilikiwa na mwekezaji anayejenga kiwanda cha saruji Mtwara
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete ametumia siku nzima ya Ijumaa, Mei 9, 2014, kutembelea kiwanda
kikubwa zaidi cha saruji kuliko kingine chochote duniani cha Dangote
Cement Obajana Plant na kinachomilikiwa na tajiri mkubwa zaidi wa
Afrika, Bwana Aliko Dangote, ambaye pia anajenga kiwanda kikubwa cha
saruji mjini Mtwara.
Akiandamana na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Abdallah
Kigoda, kwa siku nzima, Rais Kikwete ametembelea kiwanda hicho cha
Saruji cha Dangote kilichoko katika eneo la Obajana, Jimbo la Kogi,
kilomita 400 kaskazini mashariki mwa mji maarufu wa kibiashara wa
Nigeria, Lagos.
Rais Kikwete ambaye alikuwa nchini Nigeria kuhudhuria Kongamano ya
Uchumi Duniani-Afrika (WEFA) mwaka huu aliamua kutumia siku yake ya
mwisho ya ziara yake ya siku tatu nchini humo, kwa kutembelea uwekezaji
mkubwa wa mwekezaji ambaye ameanza ujenzi wa kiwanda cha saruji cha
Mtwara ambacho kitakuwa kiwanda kikubwa zaidi cha saruji kuliko kingine
chochote katika Tanzania, kikiwa na uwezo wa kuzalisha tani za kimetriki
milioni tatu kwa mwaka.
Rais Kikwete ambaye alipokewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kiwanda hicho
na Bwana Dangote mwenyewe, na kuanza ziara yake kwa kutembelea machimbo
ya kiwanda hicho ambayo yako kilomita tisa kutoka kiwandani ambako
malighafi ya kiwanda hicho husafirishwa kwa madaraja na mikada maalum
hadi kiwandani.
Bwana Dangote amemwambia Rais Kikwete kuwa kwa sasa Kiwanda cha Obajana
kinazalisha tani za kimetriki milioni 10.25 kwa sasa kwa mwaka na hivyo
kukifanya kiwanda hicho kuwa kiwanda kikubwa zaidi cha saruji duniani
kilichoko katika eneo moja na kuwa baada ya upanuzi unaoendelea kufanywa
kwenye kiwanda hicho, uwezo wake wa uzalishaji utaongezeka na kufikia
tani za kimetriki 13.0 kwa mwaka ifikapo mwakani 2015.
Bwana Dangote amemwambia Rais Kikwete kuwa kiwanda hicho kilicho kwenye
eneo la kilomita za mraba saba kitakuwa kimegharimu kiasi cha dola za
Marekani bilioni 2.5 wakati upanuzi wake utakapokamilika.
Kwa sasa kiwanda hicho kina biashara ya dola za Marekani bilioni mbili
kwa mwaka. Bwana Dangote amemwambia Rais Kikwete kuwa kiwanda hicho
kilichoanza kujengwa mwaka 2003 na kukamilishwa mwaka 2006 na hatimaye
kuzinduliwa na Rais Olusegun Obasanjo Mei 12, mwaka 2007, wiki mbili
kabla ya kustaafu Urais wa Nigeria, kinaajiri watu 800 kwa wakati mmoja
na hivyo kuwa miongoni mwa waajiri wakubwa zaidi katika Nigeria.
“Mheshimiwa Rais, ili kuelewa vizuri mchango wa kiuchumi na kijamii za
kiwanda hiki na viwanda vyetu vingine katika maeneo mengine ya Nigeria,
unahitaji kukumbuka kuwa kabla ya kuanza kujenga kiwanda hiki, Nigeria
nzima ilikuwa na uwezo za kuwazalisha tani za kimetriki za saruji
milioni1.5 tu, wakati huo chini ya miaka 10 iliyopita.
"Tunataka kufikia hatua ya kuhakikisha kuwa eneo la Afrika Magharibi na
hata Bara letu la Afrika linaacha kabisa kuagiza saruji nje ya Bara
letu. Na tutafikia huko.”
Mbali na Kiwanda cha Obajana, Kampuni ya Saruji ya Dangote inazalisha
saruji katika maeneo mengine mawili ya Nigeria ambalo uzalishaji wa
jumla wa maeneo hayo matatu ni tani za metriki 20.25 kwa mwaka. Amesema
Bwana Dangote kuwa ili kuweza kuwa na uhakika wa umeme, uongozi wa
kiwanda hicho uliamua kuzalisha umeme wake kwa ajili ya kiwanda hicho
kwa kujenga, miongoni mwa hatua nyingine, bomba ya kilomita 92 la
kusafirisha gesi kutoka Ajaokuta hadi kwenye kiwanda hicho.
Alipoulizwa na Rais Kikwete kama wanategemea kwa namna yoyote umeme wa
taifa, Bwana Dangote alijibu kwa furaha, “hatujaunganishwa kwenye gridi
ya taifa na tunadhani hili ni jambo zuri kwa sababu hatua tulizochukua
zinatuhakikishia umeme wakati wote na kwa kiwango ambacho tunakihitaji.
Tunatumia gesi ama diseli yetu wenyewe. Na wala siyo umeme tu, hata
miundombinu ya eneo hilo kiliwemo daraja hili kubwa linalonganisha eneo
la machimbi na kiwanda, tumejenga sisi Mheshimiwa Rais.”
Bwana Dangote amesema kuwa mbali na kujenga miundombinu ya umeme wake,
kiwanda hicho pia kimejenga bwawa lake lenyewe kwa ajili ya huduma ya
maji kusaidia uzalishaji wa saruji bila kutegemea huduma ya maji ya
Serikali.
Aidha, bwawa hilo linatoa huduma ya maji kwa jamii inayozunguka kiwanda
hicho. Mbali na shughuli za kiwanda, Kampuni ya Bwana Dangote inashiriki
kwa karibu sana shughuli za jamii inayozunguka kiwanda ambacho kwa sasa
imeanzishwa miji midogo saba katika eneo lililokuwa pori lenye nyumba
50 za wenyeji tu kabla ya shughuli za kiwanda hicho kuanzishwa.
Bwana Dangote amemwambia Rais Kikwete kuwa kampuni yake inatoa shughuli
za elimu, maji na umeme kwa wananchi ambao wanazunguka kiwanda ambacho
tokea kuanzishwa kwake limevutia mabenki 13 ambayo yameanzishwa matawi
yake katika eneo la kiwanda.
“Mheshimiwa Rais, mbali na nyumba za wafanyakazi, tunawajengea hata
nyumba za kuishi wananchi wanaozunguka eneo hili ambao wanatuunga mkono
sana.” Mbali na kutoa huduma nyingine za kijamii, Kampuni ya Saruji ya
Dangote inajenga taasisi kubwa ya elimu ya Dangote Academy ambayo itatoa
elimu na mafunzo ya kiufundi kwa ajili ya kuandaa wafanyakazi wa
kiwanda hicho na watoto wa jamii inayozunguka kiwanda hicho.
Ili kuhakikisha kuwa upanuzi wa kiwanda hicho unakwenda kwa kasi kubwa
zaidi, Bwana Dangote ameagiza kiasi cha malori 6,000 kutoka China
kusaidia ujenzi na pia amechukua uamuzi usiokuwa wa kawaida wa kuagiza
maelfu ya vibarua kutoka nchi hiyo hiyo ya China kushiriki katika ujenzi
huo na kuumaliza kwa haraka.
Bwana Dangote amemwambia Rais Kikwete kuwa kampuni yake inafanya
jitihada kubwa kuhakikisha kuwa Rais Kikwete anakifungua kiwanda cha
saruji cha Mtwara kabla ya kustaafu mwishoni mwa mwaka ujao.
Mbali na Nigeria na Tanzania, Bwana Dangote ana viwanda ama anajenga
viwanda vya saruji ama na shughuli za saruji katika nchi 14 za Afrika
ikiwamo Ethiopia, Zambia, Mozambique, Kenya, Senegal na Sierra Leone,
Afrika Kusini, Congo (Brazzaville), Cameroun, Ghana, Liberia na Ivory
Coast.
Mbali na shughuli za uzalishaji wa saruji, Bwana Dangote ambaye
anakubaliwa kuwa tajiri mkubwa zaidi katika Afrika kwa thamani ya dola
za Marekani bilioni 25 yeye na kampuni yake ya Dangote Group pia ina
shughuli za uzalishaji wa sukari, uzalishaji wa chumvi, utengenezaji wa
magunia, uzalishaji maji, uzalishaji wa vyakula vya aina mbali mbali,
uzalishaji wa mafuta ya kupikia, utengenezaji wa nyanya.
Kwa sasa anaendelea na ujenzi wa kiwanda cha mbolea na kile cha
kuzalisha bidhaa za petrol na kemikali. Kampuni ya Saruji ya Dangote –
Dangote Cement- ndiyo kampuni kubwa kuliko zote katika Afrika Magharibi
kwa sasa ikiwa na thamani ya dola za Marekani bilioni 22.7 kwa tathmini
ya mwaka huu baada ya kuongeza thamani yake kutoka dola za Matrekani
bilioni14.5 za mwaka jana. Mwishoni mwa ziara hiyo yenye mafanikio
makubwa, Rais Kikwete aliondoka Obajana kurejea nyumbani kupitia
Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Luanda, Angola ambako jana
Jumamosi alikutana na marais wa nchi hizo kabla ya kurejea nyumbani.
