A

A

MAKUBWA: AKUTWA AMELALA MTALONI AKIWA HANA NGUO












Mtu mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja, amekutwa leo 30/4/2014 akiwa amelala mtaroni maeneo ya Mitandi - Lindi Mjini. Mtu huyo ambaye ilifahamika ana undugu na mtu mmoja aitwaye "BUSHIRI" katika maeneo hayo alikutwa majira ya saa 2 asubuhi akiwa amelala usingizi mzito mtaroni akionekana na michubuko kadhaa usoni. Mtu huyo ambaye alinikwepa kumpiga Picha alinigomea nisimpige picha licha ya kumweleza kuwa nahitaji kumsaidia kumpata mtu aliyemchukulia nguo zake. Mashahidi wa tukio hilo walisimulia kuwa mtu huyo ambaye alioneka amelewa baada ya kuamka, alikutwa akiwa amelala fofofo na baada ya kusikia sauti za watu wakimshangaa ndipo alipozinduka na kujikuta YU UCHI na kuzuga kuwa anatafuta msala wa kujisaidia. Mashahidi hao walisema hawajui zaidi ya nini kilichompata usiku wa jana hali iliyomweka katika hali hiyo "isiyoeleweka" kama ametendwa na wahuni ama amelipishwa pombe aliyokunywa. Jamaa aliamua kujificha nyumani kwa Mudhihiri (jirani na BOMOLEA) ili kukwepa asinaswe na Camera hii. Kwa kuwa hakutaka kusema chochote na mhabarishaji nawasilisha kwenu tuzuie uhalifu wa aina hii Mjini Lindi.


Picha na Lindi yetu Blog/ Blogs za Mikoa