A

A

KINANA AWAHUTUBIA MAELFU UWANJA WA KIBANDAMAITI ZANZIBAR LEO .... WAZANZIBARI WAAPA KUULINDA MUUNGANO

  • Wananchi wa Zanzibar wasema serikali mbili zatosha
  • Wachukizwa na wanasiasa wanafiki wanaopindisha pindisha maneno
  • Vijana wa CCM kutovumilia wanasiasa wanaokashifu waasisi wa Taifa letu
  • Wasema wamechoshwa na matendo ya Viongozi wa Vyama vya Upinzani wataka muswada wa kuujadili Serikali wa Umoja wa kitaifa wataka ufutwe kwani hauna faida kwa maendeleo yao .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Zanzibar na kuwaambia CCM itasimamia haki za Wazanzibar na kuhakikisha Muungano unadumu na Mapinduzi ya Zanzibar yanaenziwa .
 Wananchi wakionyesha ishara ya Serikali mbili kwenye mkutano wa CCM kwenye viwanja vya Kibanda Maiti, Unguja Zanzibar.
Kinana akihutubia Kibandamaiti, Zanzibar leo
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia  kwenye mkutano wa hadhara wa CCM  leo, May 4, 2014, kwenye Viwanja vya Kibandamaiti, mjini Zanzibar. (Picha na Bashir Nkoromo)
1(15)
Umati uliohudhuria kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliohutubiwa na Kinana leo, May 4, 2014, kwenye Viwanja vya Kibandamaiti, mjini Zanzibar.
  2(13)
Watu wengi wakiwa wamejitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa CCM , May 4, 2014, kwenye Viwanja vya Kibandamaiti, mjini Zanzibar. 
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na watoto akionyesha ishara ya serikali mbili wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya kibanda maiti na kuwataka wanawake wote wa Zanzibar kuungana katika kusimamia Muungano wa Tanzania.
 Mbili zatosha.
 Kila mtu alionyesha mapenzi yake kwa CCM.
 Wakazi wa Zanzibar hawakujali mvua iliyokuwa inanyesha kwenye mkutano wa CCM Kibanda Maiti Zanzibar
Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume akihutubia wakazi wa Unguja na kuwaambia kuwa waasisi wetu waliweka uzio wa kutulinda na kudumisha umoja na undugu wetu na kusema uzio huo ni Muungano wetu.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mbunge wa BundaStephen Wassira akihutubia wananchi wa Zanzibar ambapo alisema UKAWA wanatakiwa kuelewa misingi ya Muungano kwanza kisha waje na hoja .

Mbunge wa Songea Mjini Dk Emmanuel Nchimbi akihutubia wakazi wa Unguja kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kibanda Maiti na kuwataka wananchi hao kuwa makini na viongozi wanaogeuza maneno huku akitolea mfano kutoka kwenye kitabu cha Maalim Seif.
Katibu wa NEC  Oganizeshen Dk. Mohamed Seif Khatibu akihutubia wakazi wa Unguja kwenye mkutano wa hadhara Kibanda maiti .

Sehemu ya Umati uliohudhuria mkutano wa hadhara ambao ulihutubiwa na Viongozi mbali mbali wa CCM wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Makamu Mwenyekiti wa UWT Bi.Asha Bakari Makame akihutibia umati uliofurika kwenye viwanja vya Kibanda Maiti  na kuwaambia Wazanzibar wanaelewa maana ya Muungano na hawapo tayari kuuvunja kwa namna yeyote.
 Viongozi wa CCM wakifuatilia kwa makini hoja mbali mbali za kujenga na kuimarisha Muungano.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amekaa pamoja na Makamu wa pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd (kushoto) Mjumbe wa Kamati Kuu na Mbunge wa Bunda CCM Ndugu Stephen Wassira ,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Borafya Silima (kulia) na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakifuatilia mkutano wa hadhara bila kujali mvua iliyokuwa inanyesha.