Hii
stori ilianza baada ya kutoka kwa jarida la Vibe Magazine ambalo
lilitoka wiki iliyopita,mbele ya jarida hilo kulikua na picha ya Ommy
Dimpoz akiwa kakaa huku miguu akionekana na mavazi ya kike,mjadala huu
ulianza baada ya kuonekana kwa viatu hivyo na wengine wakidai kuwa hata
suruali haikua ya kiume.
Ommy
Dimpoz aliongea na Dj Fetty kupitia So so Fresh ya Ijumaa mei 09,hiki
ndicho alichokisema>>’Viatu sio vya kike kwa sababuukisema viatu
vya
kike unamaanisha labda umeenda kununua kwenye duka la vitu vya kike
na viatu vile mimi nimenunua South Africa kipindi tumeenda kumsindikiza
AY kwenye Channel O’
‘Nakumbuka tena siku ambayo nimeenda kununua nilikuwa na Dulla Spatan
nilinunua kama jozi ishirini au thelethini zilikuwa jozi nyingi unajua
muda mwingine unaweza kuingia kwenye maduka ukakuta kuna vitu
vinauzwa,kwahiyo nilikuta,halafu na vile vilikuwa ni vyepesi havina
uzito’
‘kwahiyo nikanunua nunua vile vingi,lakini nimenunua kwenye Mr Price
nakumbuka, vilikuwa ni rahisi,sidhani kama watu wameichukuliaje lakini
huenda labda fashion ndio imenigharimu,lakini naona ni viatu vya kawaida
na watu wanavaa hata ukiangalia wanamitindo’
‘Hata watu wengi wanavaa kwahiyo kwa kununua mi nimenunua sehemu ya
vitu vya kiume na hakikua kimoja kusema labda wamekosea wamekiweka sehem
tofauti, ni kwamba viko vingi na aina tofauti’.