A

A

KAJALA SIMU YAKE AIONA KAMA KITUO CHA POLISI


Muigizaji wa filamu nchini Tz, Kajala Masanja amesema kutokana na ugomvi wake na Wema Sepetu ulivyokuwa mkubwa, amefikia hatua ya kuiogopa simu yake zaidi ya kupiga na kupokea.
Akiongea katika kipindi cha Take One kinachorushwa na Clouds TV, Kajala amesema amekuwa akiumizwa na kutukanwa kwenye mitandao ya kijamii kutokana na ugomvi huo.
Kajala amesema ugomvi wao haujatokana na kile kinachoongelewa kuwa alimchukulia bwana yake na kwamba umetokana na vitu vidogo vya binafsi kwao. Na amesema ugomvi wao umekuzwa na watu na media kiasi kujikuta maadui kweli, katika hayo Kajala amekili kukosana na Wema kumemuathiri katika maisha yake "Inaniathiri sana kwasababu ni mtu ambaye nimemzoea sana, mtu ambaye tumefanya vingi so nikikaa nammiss sana." alisema Kajala