A

A

HAYA SASA FID Q NA DAYNA WAINGIA KATIKA MKANGANYIKO, FID Q AMCHANA LIVE, MKOROGO NAO WAHUSIKA


fidqKutokana na sababu ambazo zilikua nje ya uwezo hukusikiliza You heard ya jana Mei 20 sikuiweka hapa ,sasa kwa kuwa nipo kwa ajili yako na sipendi upitwe na kitu,You heard ya jana ilikua inamhusu Fid Q na Dayna na Fid Q ameingia hasa utata wa kwenye line zake  kadhaa kwenye wimbo wa Sina Muda wa Jcb ambazo zimeonekana kumhusu moja kwa moja Dayna.
daynaFid Q ameonekana kama anamfokea Dayna kwa kutumia mkorogo unao badilisha ngozi yake na kuonekana mweupu kitu ambacho Fid Q amedai kuwa Dayna anaukimbia uafrika,Mistari ya Verse hiyo iko hivi.

“Hi Dayna, sikufichi ulikua unahusika/
au mtoto wa uswazi ‘ akijichubua ‘ haimaanishi anaukimbia uafrika?/
nisikize Dayna..please.. najua uko busy kiaina na hizi ni aina tu za uchizi au kama vipi bye DAYNA/
HUUH.. now back to you fools/
Soudy brown kamtafuta Fid Q ambapo alipoulizwa kuhusu hili majibu yake alidai kuwa katika ngoma hiyo hamzungumzii Dayna Msanii bali anamzungumzia Dayna msichana anayeishi nae kitaani maeneo ya Mikocheni kwa Nyerere.
Dayna huyo wa kiafrika alikua mweusi sasa hivi amejichubua ngozi yake na kuwa mweupe ambapo baadae Fid Q aliuchambua kiutaalam mstari huo na kusema kuwa wadada wanaofanya hivyo wanaua melanie.
Ambacho ni kitu muhimu sana kwenye ngozi na hupatikana zaidi kwenye ngozi nyeusi ya kiafrika chembechembe ambazo huilinda ngozi isiunguzwe na jua.
Majibu ya Dayna baada ya kupigiwa simu na Soudy Brown kutaka kujua kama ameshaisikia hiyo line ya Fid Q alichokijibu ni ameisikia na anamuheshimu Fid Q kwa wazo lake ila kwa wakati huu amepunguza kidogo kutumia mikorogo.