Baada
ya kufanikiwa sana kwa mavazi yake yaliyojulikana “Single Buttons”,
sasa mbunifu maarufu wa mavazi hapa nchini Martin Kadinda katambulisha
aina mpya ya mavazi yajulikanayo kama ”Kwachukwachu”. Aina hii mpya ya
mavazi imepokelewa vizuri sana kwani siku chache tu baada baada ya
kutambulisha mavazi hayo Diamond Platnumz aliamua kumuunga mkono kwa
kununua shati la “Kwachukwachu”. Diamond alionekana amevaa shati hilo
katika video iliyowahusisha wasanii wakubwa 19 kutoka Afrika.
Siku ya leo kupitia akaunti yake ya
Instagram, Martin Kadinda katambulisha mavazi ya Kwachukwachu ambayo
yatakua yakivaliwa na wadada. Martin aliweka picha za Wema akiwa kavaa
Gauni fupi la Kwachukwachu.