Idara ya polisi mjini New York
Marekani, imefunga kitengo chake maalum cha ujasusi ambacho huwapepeleza
waisilamu ili kuchunguza kama kuna tisho lolote la ugaidi.
Kitengo hicho kilikuwa kinatumia polisi
waliokuwa wanavalia nguo za kiraia kusikiliza kisiri mawasiliano ya simu
kati ya waisilamu na hata kuzuru maeneo yanayotembelewa sana na
waisilamu.kitengo hicho kiliwahi kushitakiwa mara mbili kwa mbinu zao za ujasusi na pia kulaaniwa na makundi ya wanaharakati wa haki za binadamu.
Pia kiliwaghadhabisha waisilamu hasa kwa kuwachunguza.
"mageuzi haya ni hatua muhimu sana katika kuondoa hali ya wasiwasi na kutoaminiana kati ya polisi na jamii ili jamii iweze kusaidia polisi kuwashika wahalifu,'' ilisema taarifa kutoka katika ofisi ya meya wa New York Bill de Blasio.
'Vita vya kisaikolojia'
Hatua ya kusitisha mpango huo, ilifikiwa na kamishna mpya wa polisi wa kituo hicho, na inaonekana kama njia moja ya kubadili mbinu za kukusanya ujasusi ambazo wengi wanasema zilichangia mashambulizi ya Septemba 9/11
Kitengo hicho, kilichoanzishwa mwaka 2003, na baadaye kuitwa, ' Zone Assessment Unit ' kilipeleleza waisilamu hasa maeneo walikofanya kazi, kuswali, kununua madukani na hata mikahwa walikokuwa wanakulia.
Wakuu wa kitengo hicho wanasema kuwa kazi yao iliathiri sana uhusiano kati ya jamii na polisi