A

A

Straika Mgambo: Mbona Ngassa anabeba hirizi hamsemi!


Straika wa mgambo Mohamed Neto Akiwania mpira na beki wa Simba William Lucas "Gallas"
STRAIKA wa Mgambo, Mohammed Neto ambaye aliondolewa uwanjani kwa kupewa kadi nyekundu katika mechi dhidi ya Yanga, amefunguka kuwa hata kama alikuwa amebeba hirizi, atakuwa amefanya hivyo kwa faida yake huku akisema mbona wachezaji wengine wakibeba hawaandikwi kwenye magazeti!
Neto ambaye katika ripoti ya mwamuzi wa mechi hiyo, Alex Mahagi na kamisaa wa mchezo, Tito Haule, iliripotiwa kuwa alitolewa kutokana na kuwa na bisibisi, amewaka kwa kusema hakuwa na bisibisi wala hirizi lakini kama ni hirizi kuna wachezaji kama kina Mrisho Ngassa wa Yanga wanabeba kwenye mechi na hawalalamikiwi.
Mshambuliaji huyo mwenye mwili mkubwa, amelalama kuwa yeye hakuwa na silaha yoyote, hivyo anashangaa taarifa kuwa alikuwa amefunga hirizi sehemu za siri.
“Mi nashangaa sana nyie watu wa magazeti mnaniandika nimebeba bisibisi, hivi inaingia akilini kweli ubebe bisibisi kisha ucheze mpira?
“Huyo mwamuzi sijui amewaza nini, hata kama nilibeba hirizi kwani kuna tatizo gani? Mbona wapo wengi tu wanabeba, hao kina Ngassa mbona hamuwaandiki kuwa wanabeba hirizi!
“Mtu anaweza kubeba hirizi kwa kuwa ni sehemu ya kinga yake, kwani, mi najua hizi ni fitina tu za magazeti kwa kuwa nyie mnazipenda Yanga na Simba au hamkutaka tuifunge Yanga? Acheni hizo bana, mwambie na huyo mwandishi aliyeandika hiyo habari mi nitamshtaki,” alisema beki huyo.