Dar es salaam imekua ikipokea mvua kubwa sana kwenye siku hizi za
karibuni ambayo imehusika sana kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kwa
watu kuonyesha jinsi madimbwi yalivyotawala hata kwenye sehemu ambazo
hazikutarajiwa barabarani.
Ukubwa wa hizi mvua ulisababisha ukungu mkubwa sana April 11 2014 mchana
wakati ndege ya shirika la Kenya na abiria 49 ikiwa inatua kwenye
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam ikitokea
Kenya.
Marubani walipata tabu wakati wa kutua hivyo ikatua kwa kishindo
kilichopelekea ishindwe kutua kwenye barabara kama inavyotakiwa na
badala yake ikaingia mpaka kwenye majani.
Polisi
ilipozungumza na Radio One, imesema ajali hiyo ilisababisha kusitishwa
kwa safari zote za ndege kuondoka na kutua huku abiria waliokuwemo ndani
ya hii wakishushwa kwa dharura kama moja ya hizi picha inavyoonyesha
hapo chini mwisho.
Sehemu ya injini ya upande wa kulia ya ndege hii iliyokua na Wafanyakazi
saba ndani yake, imeharibika kutokana na kukita chini kwa kishindo
wakati wa kutua.