Zaidi ya abiria 55 waliokuwa ndani ya
basi la kampuni ya Hood,
wakisafiri kutoka Mbeya kwenda Arusha walinusurika kufa baada ya basi
hilo kushika moto na kuteketea kabisa katika kijiji cha Kilolele,
Chalinze mkoani Pwani.
Kufuatia ajali hiyo ya moto ya basi la Hood, mpaka sasa chanzo cha moto huo hakijaelezwa.
Julai 2011, Kampuni hiyo ya mabasi ya Hood iliungua moto karibu na
hifadhi ya Mikumi mkoani Morogoro ambapo watu watano walikufa kwenye
basi hilo lililokuwa na namba za usajili T 762 AVL lililokuwa likitoka
Mbeya kwenda Arusha.
Katika ajali hiyo abiria 40 walijeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za
miili yao na kukimbizwa katika Hospitali ya Mkoa ya Morogoro kwa
matibabu.