Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akitoa salamu za chama hicho kwa Familia ya Mwalimu Nyerere, wakati vongozi mbali mbali na wabunge wa chama hicho, walipomtembela Mama Maria Nyerere (katikati) nyumbani kwake Butiama jana. Kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilibrod Slaa.
Mtoto wa tatu wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Magige Kambarage, akitoa nasaha zake kwa viongozi na wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), walipozulu katika kaburi la baba yake Butiama.
Hapa wageni ambao ni viongozi wa Chadema na
wenyeji wa familia ya Nyerere wakimwombea mwasisi huyo wa taifa.
============================== =============================
Nimejaribu kuangalia hizi picha ili nisome ujumbe ulioko ndani ya picha halafu nikafikiria mapendekezo ya UKAWA-ndani ya Bunge Maalum inayoongozwa na Mh. Mbowe na pia UKAWA-nje inayoongozwa na Dr. Slaa ambapo waliamua kukaa chini wakisaidiwa na Tundu Lissu na kuandika mapendekezo ya wajumbe wachache, baadaye wakaamua kumpa Mh. Tundu Lissu ili ayawakilishe ndani ya Bunge Maalum siku ya Jumamosi, tarehe 12 April 2014.
Mapendekezo yake yalikuwa yamejenga maudhui kuwa Mwl. Nyerere alizoea vya kunyonga katika utawala wake na hakuviweza vya kuchinja. Mwl. Nyerere alikuwa ni muongo na mdanganyifu katika utawala wake na hakuweza kusema ukweli. Mwl. Nyerere alikuwa ni tapeli na aliwatapeli wananchi kuwaaminisha kuwa wameungana wakati hawakuungana kama nchi moja mpaka mwaka 1984.
Hawa viongozi wakuu wa CHADEMA walienda kumjulia hali Mama yetu, Mama Maria Nyerere na kuhani kwenye kaburi la Baba wa Taifa wakati wanaamini ndani ya mioyo yao kuwa Marehemu Mume wake(Baba wa Taifa) katika utawala wake alikuwa ni muongo, mdanganyifu na mjanja janja ambaye hata Muungano wetu aliufanya kwa ujanja ujanja na udanganyifu na aliendelea kuwadanganya wananchi mpaka alipoaga dunia. Kwa mantiki nyingine, walienda kumsalimia Mke wa Rais ambaye alikuwa anaishi na Rais tapeli wa kisiasa.
Inaonyesha kuwa, viongozi wakuu wa CHADEMA wanamtumia Baba wa Taifa kwa maslahi zaidi ya kisiasa. Viongozi wakuu wa CHADEMA wanamuweka Baba wa taifa katika pande mbili kama sarafu. Upande mmoja wanamuita tapeli ili kuliingiza ndani ya fikra za CHADEMA kundi la baadhi ya watu wenye fikra hizo na upande wa pili wanasema ni kiongozi shupavu na Baba wa Taifa ili pia kuliingiza kundi la watu wengi wanaofahamu hivyo.
Kama kweli Baba wa Taifa alikuwa ni tapeli, kwa nini waliamua kwenda kuhani kaburi la kiongozi wanaeamini kuwa ni tapeli?. Kwa nini wanaweka picha za Baba wa Taifa kwenye ofisi na mikutano yao. Hivi ni nani mnafiki na mlaghai wa kisiasa hapa?.

Wananchiblog