Wema Isaac Sepetu aliyewahi kuwa Miss Tanzania 2006, amejitoa fahamu kwa
kupandisha mzuka na kutinga makao makuu ya Kampuni ya Global
Publishers.Alifika kwenye ofisi hizo mitaa
ya Bamaga-Mwenge, Dar-es-Salaam na kuzua timbwili la aina yake kisa
kikiwa ni kile kinachodaiwa kuandikwa kwa habari zake na mpenziwe,
Nasibu Abdul ‘Diamond’.