A

A

Mourinho:Wachezaji walipambana kama wanyama.


Meneja wa Chelsea,Jose Mourinho anaamini kuwa timu yake ilijitoa kwa kila kitu katika ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Paris Saint-Germain kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali.
Mara baada ya kuwa na maumivu ya kipigo cha goli 3-1 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Parc des Princes,goli la dakika za lala salama kupitia kwa Demba Ba liliwapeleka Chelsea nusu fainali yao ya saba katika kipindi cha miaka 11
Mourinho alionyesha heshima na pongezi zote kwa kiwango kilichoonyeshwa na timu yake na kusema kuwa anaamini kupambana kwa nidhamu yote ndiyo kuliwasaidia kuishinda klabu hiyo ya Ligue 1.
Huku akisisitiza kuwa,”Walitupa kila kitu na upinzani wa hali ya juu.Kulikuwa na baadhi ya hali ngumu katika mchezo,walitupa upinzani wote.”

“Nakuhaidi wewe,kucheza dhidi ya Lucas sio kitu rahisi.kucheza dhidi ya Cavani na Lavezzi sio kitu rahisi hata kidogo.”
Akaongeza kuwa,”Walinzi wangu wanne kama ilivyo mara zote,walikuwa katika ubora wa
hali ya juu lakini viungo walifanya kazi kama wanyama na David Luiz alikuwa mnyama mwenye hasira kali zaidi(Monster).

Mourinho alisema kuwa washambuliaji wake walijaribu kutengeneza nafasi na walicheza vizuri na hata ilipokuwa inapaswa kutumia nguvu ya mwili,Fernando Torres na Demba walionyesha msaada mkubwa sana kwa timu.

Na akadai kuwa alipaswa kuwachezesha Demba,Torres na Eto’o kwa pamoja kwasababu viungo wake walikuwa wamechoka sana na walikatika lakini pia Paris walikuwa katika hali kama hiyo hivyo walitambua itakuwa kazi kubwa kwa wapinzani wao kwendana na staili hiyo kutokana na aina ya soka la nchini Ufaransa.
Pia akakiri kuwa walicheza kwa kujitoa muhanga na mwisho walifanikiwa hivyo ni kitu cha kufurahia na kujipongeza kwa jinsi walivyoonyesha kujituma katika muda wote wa mchezo.

Mreno huyo alieleza sababu ya kumtoa winga,Eden Hazard mara baada ya dakika 18 na nafasi yake kuchukuliwa na mfungaji wa goli la kwanza,Andre Schurrle.

Alipoulizwa kama raia huyo wa Belgium alikuwa mzima,Mourinho alijibu.”Hapana.Hazard alikuwa anajisikia maumivu katika goti lake na alikuwa anasema hawezi kuendelea na mchezo