TAARIFA KWA UMMA
Naibu Waziri wa Fedha(S) Mh:Mwigulu Lameck Nchemba(Mb) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Tanzania Bara ataongoza Sherehe za Kuadhimisha Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania Kwa Watanzania Waishio Nchini Marekani-Washington-DC na Viunga Vyake.
Maadhimisho hayo yanayotegemewa Kufanyika Tar.26/04/2014 katika Ukumbi wa MATINICE EVENTS AND CONFERENCE CENTRE,7925 CENTRAL AVE,CAPITOL HEIGHTS,MD 20743.
Mh:Mwigulu Nchemba aliyealikwa na Balozi wa Tanzania Nchini Marekani Mh:Libereta Mulamula kuongoza Sherehe hizo za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano,atazungumza na Watanzania kuhusu Muungano Wetu,Kuulinda,Kuutetea na Kuudumisha kwa Manufaa ya Taifa letu la Tanzania na Watu Wake.
Watanzania Wote Mnaombwa Kufika kwa
Wingi kwenye Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhai wa Muungano Wetu,Hii ni nafasi nzuri kwa Watanzania Nchini Marekani kuandika Historia Mpya kwa Taifa letu.
Mungu Ubariki Muungano Wa Tanzania,
Mungu Ibariki Tanzania.
Imetolewa na
Ofisi ya Naibu Waziri wa Fedha(S)
Mawasiliano.
23/04/2014