Mwenyekiti
wa Kamati namba tano(5) ya Bunge Maalum la Katiba Hamad Rashid Mohamed
(katikati) akiongoza mjadala wa Kamati hiyo leo mjini Dodoma wakati
wanapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.
Mwenyekiti
wa Kamati namba kumi na moja(11) Anna Kilango akiongea na waandishi wa
habari juu ya mambo yaliyojitokeza katika kikao cha Kamati hiyo wakati
wanapitia rasimu ya Katiba mpya. Mwenyekiti
wa Kamati namba kumi(10) ya Bunge Maalum la Katiba Paul Kimiti
(katikati) akiongoza mjadala wa Kamati hiyo leo mjini Dodoma wakati
wanapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba Salehe Nassoro Juma akitoa mchango wake leo
mjini Dodoma kuhusu muundo wa muungano wakati wa kikao cha Kamati namba
nne (4) kilichokuwa kinapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba
mpya.
Baadhi
ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba ,Kamati namba nne (4) wakiwa
katika kikao leo mjini Dodoma cha kupitia vifungu mbalimbali vya rasimu
ya Katiba kwa ajili ya kuiboresha.
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati namba nne (4) ya Bunge Maalum la Katiba Dr. Sira
Ubwa Maboya (kushoto) akiongoza mjadala wa Kamati hiyo leo mjini Dodoma
wakati wanapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa
(kushoto) akijadiliana na Mjumbe mwenzake Selemani Jafo leo mjini Dodoma
mara baada ya kikao cha asubuhi cha Kamati namba kumi (10) cha kupitia
vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Anne Makinda(kulia) akitoa mchango wake leo mjini
Dodoma wakati wa kikao cha Kamati namba mbili(2) kilichokuwa kinapitia
vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba Machano Othman Said akitoa mchango wake leo
mjini Dodoma kuhusu muundo wa muungano unaofaa wakati wa kikao cha
Kamati namba nne (4) kilichokuwa kinapitia vifungu mbalimbali vya rasimu
ya Katiba mpya.
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba Joseph Selethin akitoa mchango wake leo mjini
Dodoma kuhusu muundo wa muungano unaofaa wakati wa kikao cha Kamati
namba tano (5) kilichokuwa kinapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya
Katiba mpya. Mwenyekiti
wa Kamati namba tano (5) Hamad Rashid Mohamed akiongea na waandishi wa
habari juu ya mambo yaliyojitokeza katika kikao cha Kamati hiyo wakati
wanapitia rasimu ya Katiba mpya.
Baadhi
ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba , Kamati namba tano (5)wakiwa
katika kikao leo mjini Dodoma cha kupitia vifungu mbalimbali vya rasimu
ya Katiba kwa ajili ya kuiboresha.
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa (kulia)
akisamiliana na wajumbe wenzake leo mjini Dodoma mara baada ya kikao
cha asubuhi cha Kamati namba kumi (10) cha kupitia vifungu mbalimbali
vya rasimu ya Katiba mpya.
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba Zendi Mvano Abdallah akitoa mchango wake leo
mjini Dodoma kuhusu muundo wa muungano unaofaa wakati wa kikao cha
Kamati namba kumi (10) kilichokuwa kinapitia vifungu mbalimbali vya
rasimu ya Katiba mpya.
**********
Na Magreth Kinabo – Dodoma
Kamati
12 za Bunge Maalum zimeaanza kazi vizuri ya kuchambua Rasimu ya
Katiba, huku baadhi ya wenyeviti wakisema kuwa muda wa siku mbili wa
kujadili sura ya kwanza na ya sita hautoshi.
Hayo
yamebainika katika mahojiano ya Mwenyekiti wa Kamati namba 11 ya
Bunge hilo, Anne Kilango Malecela, yayofanyika katika ukumbi wa mikutano
wa St. Gasper mjini Dodoma.
“
Tatizo lililojitokeza ni kwamba muda wa siku mbili hautoshelezi , leo
tumejadili sura ya kwanza sehemu ya kwanza kesho tutajadili sehemu ya
pili ya sura ya kwanza hivyo tunaweza tusiiguse sura ya sita.
“
Wenzetu walikakataa Kanuni zisirekebishwe. Lakini wenzetu wapinzani
wameliona hilo wameanza kusema muda hautoshi,” alisema Anna .
Aliongeza
kuwa kutokana na hali hiyo atamweleza Mwenyekiti wa Bunge Maalum la
Katiba, Samwel Sitaa (leo jioni ) kuwa muda hautoshi.
Mwenyekiti
huyo tatizo lingine lililojitokeza katika kamati yake ni baadhi ya
wajumbe kutokuwa na uelewa wa tofauti ya dola na nchi, hali iliyomfanya
kutumia kanuni namba 56(7) kumwomba Mwenyekiti wa Bunge hilo
ikiwezekana kumleta mtaalamu wa sheria ili kuweza kutoa elimu hiyo
leo (jioni) juu ya masula hayo.
Akizungumzia
kuhusu mjadala alisema wajumbe wote walijitayarisha vizuri na
walishindana kwa hoja hivyo hakuna aliyetoa maneneo makali.
Akizungumza
kwa njia ya simu na waandishi wa habari nje ya ukumbi huo, kwa sababu
alikuwa katika Mwenyekiti wa Kamati namba moja ,Ummy Ali Mwalimu
alisema wajumbe walichangia kwa utulivu.
Ummy
alisema kilichojitokeza katika kamati yake ni kuwa muda hautoshi kama
ilivyodaiwa na baadhiya wajumbe kutoka upinzani, chama tawala na kutoka
201.
Naye
Mwenyekiti wa Kamati ya namba tano ya Bunge hilo ,Hamad Rashid
alisema kamati yake mjadala unaendelea vizuri na ulikuwa wa kistaarabu.