Ni mtoto Satrin Osinya ambae mama yake mzazi aliuwawa kwenye shambulio lililofanywa kanisani huko Mombasa Kenya ambapo watu waliokua na silaha walishambulia kwenye ibada ikabidi mama amkinge mtoto, ikisemekana risasi iliyofyetuliwa ikamuua mama na kupenyeza mpaka ikagota kichwani kwa mtoto aliebaki hai.
Satrin
mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi sita alibaki na hiyo risasi
kichwani toka shambulio hilo lilipotokea zaidi ya wiki moja iliyopita.
1.
Madaktari katika hospitali ya Kenyatta Nairobi Kenya wamefanikiwa
kuitoa risasi hiyo April 1 2014 baada ya kazi ya dakika 180 ambapo sasa
mtoto huyu hayupo tena kwenye hatari ya kupoteza maisha.
2. Kikundi cha Madaktari 12 bingwa wa kichwa ndio kimeifanya hii kazi.
3. Madaktari wanasema mtoto huyu ameanza kuongea, kucheza na hata kusogea tofauti na mwanzo.