Diamond kama kawaida yake tena kuzidi ku-shine na wakati huu kuingia
tena si kwingine, katoboa hadi kwenye tuzo maarufu za MTV zijulikanazo
maarufu kama MTV Africa Music Awards (MAMA).
Bendera ya Tanzania inazidi kupeperushwa kimuziki na Diamond Platnumz
huko kwenye tuzo hizo,Diamond platnumz ndiye msanii pekee kutoka
Tanzania aliyefanikiwa kuchaguliwa kuwania tuzo hizo, tena
katika
categories mbili, Best male na Best collaboration kupitia ‘Number One’
(Remix) liyemshirikisha Davido kutoka Nigeria, ameweka historia ya kuwa
kama msanii aliyeweza kushika kasi ya mafanikio katika kipindi kifupi,
na inavyoonyesha nikuwa nyota yake kuzidi ku-shine siku hadi siku, bila
kupumzika na hivi sasa amevuka border hadi huko jijini Johannesburg,
South Africa ilipofanyika nomination za tuzo hizi za MTV Africa Music
Awards (MAMA).
MTV Africa Music Awards (MAMA) ni kati ya tuzo zinazoheshimika sana
duniani na Africa kwa ujumla, tuzo hizi za kusheherekea wanamuziki na
mafanikio ya wasanii na watu mbalimbali, tuzo hulenga hasa wale
wanaliofanikiwa kuwagusa vijana wengi africa kimuziki na kukubalika
zaidi, watu waliochangia na kufanikiwa kufanya mabadiliko makubwa katika
jamii hasa kwa vijana kwa mwaka mzima.
Mbali na Diamond Platnumz, mTanzania mwingine aliyeweza kufika na
kupeperusha bendera ya Tzee kwenye tuzo hizo, ni mbunifu maarufu mbongo
aishie huko nchini SouthAfrica Anisa Mpungwe, huyu ni moja wa wabunifu
anayefanya vizuri duniani kwa sasa, na baadhi ya nguo zake huuzwa katika
maduka mbalimbali makubwa nchini south Africa,ikiwemo maduka maarufu ya
Mr.Price, Anisa yuko kwenye category isiyohusika na muziki, yupo kwenye
kundi moja na mtayarishaji maarufu wa video kutoka Nigeria Clarence
Peters aliyetengeneza video ya Diamond platnumz, Mynumber1 remix.