A

A

KINANA AANZA KWA KISHINDO ZIARA YAKE MKOANI KATAVI

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kushoto) akikagua ujenzi wa bandari ya Karema wilaya ya Mpanda ambao umekwama kwa miaka mitatu sasa kutokana na mkandarasi kudaiwa kutokuwa na sifa na uwezo wa kukamilisha ujenzi huo. Kinana ametembelea ujenzi huo leo akiwa katika ziara ya siku nne mkoani Katavi kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua.
 Kinana na Nape (kulia) wakitoka kukagua ujenzi wa bandari hiyo leo
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na waandishi baada ya kukagua ujenzi wa bandari hiyo ambapo ameahidi kuiagiza serikali kuhakikisha ujenzi huo ambao umekwama unakamilika
 Vijana wakitumbuiza kwa matarumbeta kumlaki Kinana Ofisi ya CCM Kata ya Karema leo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa soko la samaki la Ikola wilayani Mpanda mkoani Katavi
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa soko la samaki la Ikola wilayani Mpanda mkoani Katavi
 Kinana akikagua eneo la Mwaloni huo
 Mjumbe wa NEC, Balozi Ali Karume akizungumza na wananchi kwenye mwalo wa Ikola
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akizungumza na wananchi baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Mwalo au soko la samaki la Ikola wilayani Mpanda
 Wananchi wa Ikola wakimshangilia Kinana katika mkutano aliofanya baada ya kukagua ujenzi wa mwalo wa Ikola wilaya ya Mpanda mkoani katavi
 Mkazi wa Ikola akiwa na samaki aina ya kambale wakati akitafuta wateja katika eneo hilo la ikola wakati Kinana alipokuwa akikagua ujenzi wa soko la samaki au mwalo katika eneo hilo leo 
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza katika kikao kilichofanyika kwenye shina namba mbili, tawi la Ikola Store. Wapili kulia ni Mjumbe wa Mwenyekiti wa shina hilo, Kawawa Mustafa. Picha zote na Bashir Nkoromo wa CCM BLOG