#HABARI UKAWA watishia kuandamana
Umoja wa viongozi wa katiba ya wananchi (UKAWA) umetishia kuanzisha
maandamano makubwa hadi ikulu, endapo Rais nchini na Mwenyekiti wa Tume
ya kurekebisha daftari la wapiga kura, hawatafanya marekebisho kabla ya
chaguzi zijazo.
Hayo yamesemwa na makatibu wakuu wa vyama vya
upinzani nchini, kikiwemo chama cha CHADEMA, CUF na NCCR, ambapo
wamesema watanzania milioni tano na laki nane hawana vitambulisho vya
kupigia kura.
Vyama hivyo vimewataka viongozi husika, kufanya jitihada za kurekebisha daftari hilo, ili chaguzi zijazo ziwe za huru na haki