MKALI katika anga la sinema Bongo, Jacqueline Wolper ameangusha sala nzito kumkumbuka marehemu Steven Kanumba.
Wolper
alifanya maombi hayo juzi Jumatatu ambapo sala hizo alizifanya nyumbani
kwake, kisha akaelekea katika kaburi la Kanumba, Kinondoni jijini Dar
kumalizia maombi yake.
“Ni
mhimili mkubwa katika tasnia yetu, hatuna budi kumuombea huko aliko
aendelee kupumzika kwa amani, mbele yake nyuma yetu,” alisema Wolper.