Picha hii ni kutoka kwa mama yake wa kufikia ama mlezi ambaye ni mke wa mtume Elisha Muliri ambaye ndiye alikuwa mume wa hayati Angela Chibalonza. Angela bado anakumbukwa na ataendelea kukumbukwa kutokana na alama kubwa aliyoacha kupitia uimbaji wake katika kumtangaza Kristo kupitia album zake mbalimbali.
Hapa Baby wonder akiwa na mama yake mdogo Tete Meshak mdogo wa Angela Chibalonza ambaye pia ni mwimbaji kama alivyokuwa dada yake. Picha ni mali ya Tete. |
Hebu tumalizie mwaka kwa kusikiliza wimbo huu "Wewe ni mwema" kutoka kwake marehemu Angela Chibalonza Muliri kati ya nyimbo ambazo zinabariki kuzisikiliza kutokana na sauti, upako na mpangilio wa vyombo kwa ujumla bila kusahau maneno yake. Barikiwa