A

A

Hili ndio Onyo kali walilopewa Ukraine Kutoka kwa Urusi Mapema hi leo


Balozi wa Urusi ameonya Ukraine dhidi ya kutumia nguvu.
Kumekuwa na Malumbano baina ya Ukraine na Urusi katika Umoja wa Mataifa huku kila upande ukimshutumu mwenzake kuwa gaidi
Katika kikao cha dharura cha baraza la
usalama la Umoja wa Mataifa, balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa , Vitaly Churkin, amesema Ukraine inaandaa vita kwa watu wake mashariki mwa nchi hiyo .
Naye mwakilishi wa Ukraine , Yuriv Sergeyev, akajibu kauli hiyo kwa kudai kuwa Urusi ina njama za kuyumbisha Ukraine na kuiangusha
Akizungumza katika kikao hicho ,balozi wa Marekani Samantha Power ameishtumu Urusi kwa kuhusika katika machafuko kwa kueneza propaganda na kupeleka majeshi yake nchini Ukraine.
Urusi iliomba kuwepo kikao hicho cha baraza la usalama baada ya Rais wa mpito wa Ukraine Oleksandr Turchynov kusema kwamba angetumia nguvu kuyatimua makundi ya wapiganaji yanayounga mkono Urusi kutoka maeneo ya
majengo ya serikali iwapo hayatakua yameondoka kufikia leo asubuhi.
Amesema Ukraine haitaruhusu Urusi kutwaa maeneo yake kama ilivyofanya katika eneo la Crimea mwezi uliopita.
Balozi wa Urusi ameonya Ukraine dhidi ya kutumia nguvu.
Katika hotuba ya runinga, rais huyo wa muda amesema kuwa hatokubali kuona kilichofanyika Crimea mwezi uliopita kikirudiwa tena nchini mwake.
Huku hayo yakijiri ,Urusi imelaani tahadhari hiyo ya Bwana Turchynov , ikiishutumu serikali ya Ukraine kwa kutangaza vita dhidhi ya watu wake .
Urusi imepinga vikali tetesi za Marekani na Ukraine kuwa ndiyo inayochochea ghasia hizo na uasi katika miji iliyoko mashariki mwa Ukraine .
Ghasia na taharuki imetanda kote katika miji iliyoko mashariki mwa Ukraine huku waasi wakivamia majengo ya polisi na serikali wakiwa wamejihami kwa silaha kali.
Wapiganaji wanaounga mkono Urusi, wengi wao waliokuwa wamejihami, wanaendelea kushikilia majengo ya serikali mjini Slaviansk .
Wanahabari wa BBC waliokwenda Slaviansk, wamesema kwamba waasi wanaunga mkono kujiunga na Urusi wamejenga vizuizi na kuasha moto barabarani usiku kucha.
Picha za mtandao zaonesha ufyatulianaji risasi uliotokea wakati wa uvamizi huo wa vituo vya uma.
Afisa mmoja wa Ukraine anasemekana kupigwa risasi na kuuwawa.
Mjini Kharkiv, watu hamsini wamejeruhiwa huku makabiliano makali yakishuhudiwa katika mji wa Zapolrizhya.