Mwishoni mwa wiki iliyopita tulishuhudia project ya kipekee
kuwahi kufanywa na wasanii wa Tanzania ambapo Juma Nature, Profesa Jay
na Jay Mo walionekana kwenye kionjo cha video ya wimbo wa ‘JWTZ’ wakiwa
wametupia gwanda za kijeshi huku wakiwa na kikosi halisi cha jeshi la
wananchi Tanzania JWTZ.
Mike T, ambaye ni mmoja kati ya wahusika wakuu au organiser mkuu wa
mradi huo akiwa na P Funk Majani, ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa
project hiyo hivi sasa inamilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
“Mmiliki wa ile project sasa hivi ni JWTZ wenyewe. Kwa sababu sisi
tulipeleka idea, kwanza audio ilikuwa ni idea ambayo ni ya P-Funk kwa
hiyo kwenye kui-visualise idea ni ya kwangu. Kwamba watu wameshaimba
sawa, kwenye upande wa visual mimi nafanya nini. Kwa hiyo kila mtu
alihusika kimpango wake.” Mike T ameiambia tovuti ya Times Fm.
Mnyalu ameeleza kuwa lengo la kuhakikisha ujumbe na historia ya JKT
na JWTZ uwafikie vijana wengi ili wakiendelea kukua wawe wana ufahamu
juu ya majeshi haya na vitu vingi vizuri yanayofanya.
Kupata nafasi ya kushuti na magwanda halisi ya kijeshi na kupewa
sapoti ya kijeshi haikuwa kitu kirahisi kwa Mike T na wenzake hasa
ukizingatia kuwa maeneo mengi ya jeshi hayarusiwi kupigwa picha.
“Mchakato kweli ni story ndefu, tumehangaika ila…yaani kifupi kwamba
tunaweza kusema sasa hivi tumefungua njia tumejua njia yaani zote.
Unajua zamani ile tumefanya wakati wengine tuko East Coast tulivyotumia
kombati nini kilitokea. Yale makosa ndio yalinifunza mbele niweze
kufanya kitu gani. Yaani ni story ndefu, tumekutana na mambo mengi na
mpaka sasa hivi mambo mengi bado hayajatulia yaani upepo hapa katikati
haujatulia. Ingawa project haijaisha lakini bado kuna mambo mengi.”
Ameeleza kuwa baada ya kupewa ruhusa ya kushuti alijikuta ameshuti
vitu ambavyo haviruhusiwi na kwamba walipokuwa wanakagua walimtaka
avitoe. Zoezi la ukaguzi wa video hiyo kwa mujibu wa Mike T lilirudiwa
zaidi ya mara 9 huku vitu vingi vikiondolewa.
Hata hivyo utaratibu huo mgumu ulimfunza mengi Mike T ambaye anadai
kuwa hivi sasa anafahamu nini cha kufanya na hata naweza kuwaelekeza
wasanii wengine utaratibu wa kupata nafasi kama hiyo ikiwa ni pamoja na
waigizaji.
“Project imeisha ila kuna mambo mengi sana ila tunaweza kusema kwamba
tumefungua njia kwa watu wengine ambao watahitaji vitu kama vile
wanawaweza wakatinitafuta tukakaa yaani nikawapa steps kwamba hiki kitu
ABCD unaweza kufanya hivi. Kwa sababu kuna vitu ambavyo tulishuti
ambavyo haviruhusiwi kuonekana. Kwa hiyo nayo iliniletea matatizo sana.
“Mwisho wa siku tuseme kutokana na yale makosa nimejua vitu vingi
sana. Kwa hiyo mtu mwingine anaetaka kuja kufanya movie kutumia nini
zile then nitampa utaratibu nini kinafanyika huko. Ukiangalia wenzetu
huko Marekani wanatumia kombati wanafanya nini. Ilikuwa tatizo ni kwetu
tu. Sio kwamba wanakataza lakini utaratibu tulikuwa tunatumia ambao sio
mwanzoni.” Mike T amefafanua.