Stori: Mwandishi Wetu
NYOTA wa sinema za
Bongo, Wastara Juma ameibuka na kusema kuwa, kuna mwanaume asiyependa
mafanikio yake kiasi kwamba alifurahia alipopata ajali na kuvunjika
mguu, mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ kufariki dunia na akatangaza kwamba,
mwanaume yeyote atakayemuoa atakufa kama Sajuki.
Wastara Juma.
Katika mahojiano maalum
na gazeti hili juzi, Bamaga - Mwenge, jijini Dar es Salaam, Wastara
alisema mwanaume huyo aliwahi kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi miakka
ya nyuma, wakamwagana.
Wastara aliyasema hayo
baada ya kupigwa swali kwamba, kuna madai kifo cha mumewe, marehemu
Sajuki kilikuwa na mkono wa mwanaume aliyewahi kuwa mpenzi wake (jina
tunalishikilia kwa sasa).
“Ni kweli kuna mwanaume niliwahi kuwa na uhusiano naye, alitangaza kwamba yeyote atakayenioa atakufa kama aliyokufa Sajuki.
“Ukiachana na Sajuki,
nilipopata ajali mwaka 2009 nikavunjika mguu na kukatwa, huyo mwanaume
ambaye tulishaachana siku nyingi, alitangaza kwa watu kwamba yeye
alitaka nivunjike miguu na mikono yote ili niwe kama boksi,” alisema
Wastara huku akilengwa na machozi.
Risasi Jumamosi: Sasa Wastara, kama hali ni hiyo wewe ulichukua uamuzi gani?
Wastara: Nilikwenda kumripoti Kituo cha Polisi Oysterbay (jijini Dar).
Risasi Jumamosi: Okay, lakini unaonaje madai kwamba, huyo mtu anahusika na kifo cha Sajuki?
Wastara:
Kusema kweli mimi siwezi kujua maana Sajuki aliumwa namuona, akazidiwa
ikafika mahali Mungu akamchukua. Sasa kama ni mkono wa huyo mwanaume
sijui ila ilivuma hivyo.
Risasi Jumamosi: Lakini kwa tangazo lake hilo, wewe umejipangaje? Maana wanaume watakuwa wanakuogopa!
Wastara: Kama yeye
amejipanga iwe hivyo, hata mimi nimejipanga pia. Sina wasiwasi, lakini
namtangaza huyo mwanaume kama adui yangu namba moja. Sina wasiwasi,
siwezi kudhurika na wala mwanaume atakayenioa hawezi kudhurika.
Hayo ni maneno yake,
akae nayo tu. Kama anataka vita, nipo tayari lakini siku zote mimi ni
mkimya ila mtu akinikorofisha huwa nacharuka hasa.
Risasi Jumamosi: Tangu mmeachana na huyo mwanaume umewahi kukutana naye popote?
Wastara:
Sikumbuki kwa kweli. Nadhani sijawahi kumwona ila yupo. Amekuwa adui
hata wa familia ya kwetu kwa ajili ya matamshi yake hayo.
Risasi Jumamosi: Kwani kuachana kwenu kulitokana na nani?
Wastara:
Mimi nilimchoka kwa tabia yake. Alikuwa hajatulia. Mbaya zaidi
manyanyaso yalikuwa kila siku. Sijawahi kufurahia uhusiano wangu na yeye
-GPL
