Naitwa prosper kingu kutoka Mtui Mbeli wilaya ya Kiteto mkoani Manyara nimeokoka na BWANA YESU ni tegemeo langu la uzima wa milele.
Nina mke na watoto watano, nimeona shuhuda maisha ya ushindi blog na mimi kwa sababu matukio ya kutisha yameshanitokea, ndio maana nimekutumia na namba yangu ya simu nimekupa, ili ukweli huu ndugu zangu duniani wauone.
Tumeishi kwa amani na familia yangu hadi ubaya huu ulipoanza.
Ilianza vituko nyumbani, siku ya kwanza nijikuta nimelala chini nikajiuliza imekuaje niwe chini? nikarudi kitandani na baadae nikamsimulia mke wangu ambaye hakuelewa kilichotokea japo tulikua kitanda kimoja, nikajua ni mzaha tu.
Baada ya wiki moja vituko vikazidi, hali ya maisha yalikua magumu sana katika kijiji chetu na
siku moja tulilala bila taa kwa sababu hatukua
na pesa ya kununua mafuta ya taa, lakini usiku tukakuta taa inawaka,
imejaa mafuta na kiberiti kipya mezani. tuliogopa sana lakini nilijua
itaishia hapo. cha ajabu siku iliyofuata baada ya chakula cha usiku
tuliingia kitandani na mke wangu nilivaa bukta na mke wangu alikua
anataiti tu.
Usiku wa manane tukajikuta tupo uchi kabisa. na mke wangu amevishwa shanga kiunoni na moja ya shanga ina hirizi kubwa kama kidole gumba cha mkono, nikashangaa sana na kuhofu mno tukashauriana na mke wangu kwenda kufanyiwa maombi kanisani. Palipokucha zile shanga na hirizi hazionekani, kutokana na ugumu wa maisha nilikimbilia kwanza kazini na nilirudi saa 10 jioni, nimechoka sana nikajipumzisha kwenye kochi na usingizi ukaanza kunichukua. mke wangu akanisistiza kwenda kwa mchungaji kuombewa. Nikaanza kumpigia simu mchungaji, ila sio mchungaji kwa sababu mchungaji wangu alikua masomoni, ilikua saa 1 usiku.
Mchungaji akaniambia njoo utanikuta kanisani. nikaondoka.
Usiku wa manane tukajikuta tupo uchi kabisa. na mke wangu amevishwa shanga kiunoni na moja ya shanga ina hirizi kubwa kama kidole gumba cha mkono, nikashangaa sana na kuhofu mno tukashauriana na mke wangu kwenda kufanyiwa maombi kanisani. Palipokucha zile shanga na hirizi hazionekani, kutokana na ugumu wa maisha nilikimbilia kwanza kazini na nilirudi saa 10 jioni, nimechoka sana nikajipumzisha kwenye kochi na usingizi ukaanza kunichukua. mke wangu akanisistiza kwenda kwa mchungaji kuombewa. Nikaanza kumpigia simu mchungaji, ila sio mchungaji kwa sababu mchungaji wangu alikua masomoni, ilikua saa 1 usiku.
Mchungaji akaniambia njoo utanikuta kanisani. nikaondoka.
Kumbe wakati naenda kanisani nilitekwa njiani bila kujua. Nikizani naenda kanisani kumbe lah! nikaingia kwenye ofisi niliyodhani ni kanisani na kwa akili yangu ya kibinadamu na uenyeji wangu pale nilidhani ni kanisani kumbe hata sijui ufahamu wangu ulikua umechukuliwa maana kilichotokea ni cha ajabu mno. Nilipokaribia ofisi ile, mbele yangu nikamuona mtu kama mchungaji niliomhitaji, akaniuliza prosper umekuja? nikamjibu ndio mchungaji. Nikaingia ndani na mlango ukajifunga pale pale yule niliodhani ni mchungaji akawa binti mzuri wa kiarabu na mazingira yakabadilika ghafla, pakawa na sofa za nguvu na marashi yakuvutia.
Niliogopa sana lakini yule binti alinibembeleza na kutaka niseme chochote ninachotaka atanipa. nilichukua muda kumjibu. baada kama dakika 5 nikasimama ili nitoke nje lakini mlangoni nikakuta watu wawili wakanizuia nisitoke, sikua mbishi nikarudi kwenye sofa. yule binti akaanza manjonjo ya kimapenzi, akavua nguo zote na akanivua nguo zote, tukabaki uchi, akanikalia mapajani na kunibembeleza niseme ninacho kitaka atanipa. Nililia sana, nikawaza familia yangu, kanisa, majirani na mambo mengi yanayo nizunguka. ukweli ni kwamba maisha yangu yalikua duni sana. lakini sikuwaza utajiri wa dunia hii. Niliwaza maisha ya milele baada kufa. Nilijua huo ndio utakuwa mwisho wangu maana dakika chache baadae ningekufa na nilijua nipo kuzimu.
Nilijuta makosa niliyo yafanya duniani. sikumjibu yule binti kwa muda wa kama dakika 90, baadae nikapata ujasiri kidogo. Nikamuuliza. Namtaka YESU akanijibu "hapatikani hapa" nikamwambia "Sihitaji chochote zaidi ya YESU" Nikaanza kuomba kwa sauti ya chini, nikazidi kupata ujasiri. nikasimama kuelekea mlangoni sikuona aliyenizuia tena, nikatoka nje ya lile jengo na kuelekea nisipo pajua. kwa mwendo wa kama masaa mawili ila nikiwa uchu bila nguo hata moja maana wakati nasimama kuondoka hata nguo zangu sikuziona. Ndipo nikajua kumbe nipo mwisho wa mji na nyumbani kwangu una mwendo wa nusu saa. lakini nipo uchi kabisa huo na ni kama saa 8 usiku, mwezi unawaka maana hakukuwa na wingu kabisa muda ule. Nilijisemea moyoni kwamba, naenda nyumbani nitakayekutana nae njiani yeye ndiye mchawi, sio mimi na sipiti uchocholoni, nikaanza safari hiyo ya kwenda nyumbani.
Nilipokaribia nyumbani nikasikia mke wangu na watoto wanamwomba MUNGU maombi ambayo sio ya kawaida. Nikasimama nje nikashiriki maombi na familia yangu kwa muda kama wa dakika 10, nikagonga mlango na kumwambia mke wangu aje na kanga kwa sababu niko uchi. Mke wangu akazuia watoto wasitoke, akanisitiri kwa mavazi ndipo nikaomba niwaone wanangu.
Ilikuwa ni usiku wa majonzi sana siku hiyo na cha ajabu wakati wa matukio ya kule kwenye jengo la ajabu, mke wangu alikuwa anatumiwa sms kutoka namba ya kiarabu na maneno ya kiarabu kujurishwa kinachoendelea akaomba msaada kwa kijana mmoja mmoja mlokole ambaye walianza kuomba pamoja, lakini baadae yule kijana aliondoka kurudi nyumbani, lakini alianza tu safari kutoka kwangu, nyuma yake kulikuwa na watu wakimfuata hadi nyumbani kwake. Alipofika akamhadithia mke wake kisa cha kuchelewa, alipokuwa akimsimulia mke wake wakaanza kusikia wanapita juu ya nyumba yao wakiongea lugha isiyoeleweka, yalikuwa ni majini maana hawakulala siku hiyo bali walikesha wakiomba hadi asubuhi walipojiandaa kwenda kanisani, na walipofika kanisani yule kijana ilibidi atoe ushuhuda wa mambo yaliyotokea usiku. Kanisa likaomba na yule kijana akaambiwa apige magoti ili aombewe lakini alishindwa maana miguu yake ilikuwa inauma sana kama, alianza kuona magoti yake yanachomwa na sindano ila hakuwaona wachomaji, mambo yalipokuwa magumu aliwaeleza wana maombi tatizo hilo na hakika ilikuwa ni huzuni kanisani maana kila mmoja alishangaa na kushtuka sana. Baadae mimi na familia yangu tulifika kanisani lakini kwa sababu nilikuwa na majonzi sana sikuweza kushuhudia bali kulia tu maana nilikuwa nalia kama nimefiwa.
Lakini kwa maelezo machache niliyoyatoa kanisa lilichukua mzigo wa kufunga siku 3 bila kula usiku na mchana. Baada ya maombi hayo kumalizika nilikuwa bado niko kanisani alikuja mwanangu wa darasa la 7 Irene Prosper kutoa taarifa kwamba amezikuta nguo zangu chini ya kitanda alipokuwa akifanya usafi. Ndipo kanisa likazidi kuomba kwa bidii baada ya kuona dalili za ushindi. Siku ya jumamosi ilikuwa ni siku ya kumpokea mchungaji wetu akitoka masomoni. Mchungaji Denis Majelanga alipokuta kanisa lina pigo alitangaza maombi ya siku 7 ya kupokezana. Ndipo nilipoona ushindi wa ajabu sana kutoka kwa MUNGU, Maana katikati ya mataifa na kijiji chote cha matui kikajua kweli kwamba yupo MUNGU katika waliookoka.
Mama mmoja aliyekuwa na ukaribu sana na mke wangu alipoteza line yake ya simu , ikaokotwa na fundi mmoja wa nguo, alipojaribu kuiweka kwenye simu yake aligundua kuwa mwenye hiyo line ana mawasiliano na watu wasioishi katika hii dunia, na watu hao wasioishi katika hii dunia walikuwa wakimtaka yule mama aliyepoteza line kwamba anakikishe ananiteka na kufanya mapenzi na mimi ili nianguke katika wokovu. Kwenye hiyo line kulikuwa na meseji alizotumiwa ili afanye mazingaombwe ya kuhakikisha zoezi la kuninasa, na mipango yote ilifanyika hadi nafika kwa yule binti wa kiarabu(kuzimu) ni yeye aliifanya. Huyo mama baada ya kugundua amepoteza hiyo line na imeokotwa aliondoka hadi kwa mchungaji Denis kumuomba / kutuomba msamaha juu ya yote aliyoyatenda na alikiri kwamba yote yaliyotupata ni yeye ndio mhusika mkuu.
Mchungaji alikuja nyumbani na huyo mama, alipotoa maelezo yake! Jamani nilikosa pozi na kuwaza tu kwamba kweli ‘’dunia ina mambo.’’ Kumbe kuna watu wanaendeshwa na rimoti za kuzimu. Baada ya maelezo ya mchungaji, nilimsamehe yule mama ila nilimsihi aokoke, na siku hiyo akaongozwa sala ya toba upya. Na kuokoka upya licha ya kuwa mshirika wa miaka mingi ila kumbe hakuwa na ushirika na BWANA wetu YESU KRISTO ila alikuwa na ushirika na majini.
MUNGU awabariki sana na akubariki sana Mtumishi wa Maisha ya ushindi kwa kuuweka ili watu waone yaliyonikuta.
Namba yangu ya simu ni 0766193542 kwa yeyote atakayetaka nimusimulie live ,maana nimefupisha tu kwa baadhi ya maeneo ila uweke hivyo hivyo ila kuhusu picha siku nikipata mtu anayetumia fecebook nitakutumia ili uweke na picha.
Amen amen amen
Kutoka Maisha ya ushindi blog
Ubarikiwe sana mtumishi na asante kwa kushuhudia ili tumtukuze MUNGU pamoja, Biblia inasema kwamba ‘’Aliye na Mwana wa MUNGU, Hakosi ushuhuda’’
Tena tunamshinda shetani kwa damu ya Mwanakondoo YESU KRISTO na kwa neno la ushuhuda(Ufunuo 12:11).
Songa mbele na tuko pamoja na pia kama kuna mtu unayemfahamu anaushuhuda wa kweli nijurishe ili tuendelee kumwaibisha shetani.
KUSHUHUDIA NI KUMWAIBISHA shetani.
UBARIKIWE SANA
