Tambwe ambaye ni raia wa Burundi amesisitiza kwamba angekuwa na
wachezaji hao mpaka sasa angekuwa amepachika mabao mengi na kazi yake
ingekuwa rahisi zaidi tofauti na sasa ambapo amekuwa akitumia nguvu
nyingi zaidi Simba kutokana na aina ya uchezeshaji.
Yanga mara nyingi inawachezesha mawinga wenye kasi ambao ni Simon
Msuva, Hamis Kiiza na Emmanuel Okwi huku washambuliaji wa kati
wakisimama Didier Kavumbagu, Mrisho Ngassa wakati mwingine Said Bahanuzi
ambaye hana uhakika wa namba kikosini.
Tambwe alisisitiza licha ya upinzani wa Simba na Yanga lakini mtu
akifanya kitu kizuri kiuanamichezo husifiwa, alisema kuwa mawinga wa
Yanga wana uwezo mkubwa wa kupiga krosi na kutengeneza pasi nzuri za
kufunga mabao.
“Ujue siku zote katika mechi zetu, mara nyingi utanikuta nipo katika
eneo la
18 nikisubiria pasi na krosi kutoka kwa mawinga na viungo wenye jukumu la kunichezesha ikiwemo kunipa pasi na krosi nzuri za kufunga mabao.
18 nikisubiria pasi na krosi kutoka kwa mawinga na viungo wenye jukumu la kunichezesha ikiwemo kunipa pasi na krosi nzuri za kufunga mabao.
“Vitu ambavyo sivipati kwa ubora unaostahili Simba, ninaamini kama
timu yangu ingekuwa na mawinga wazuri kama wa Yanga wenye uwezo mkubwa
wa kupiga krosi na pasi nzuri za kufunga, basi ningefunga mabao mengi
hadi sasa katika Ligi Kuu.
“Kiukweli kabisa tuweke pembeni upinzani wetu, ninaipenda sana
kombinesheni na aina ya uchezaji wanayoitumia Yanga ndani ya uwanja,
ujue mimi kazi yangu kufunga mabao, hivyo ni lazima nipewe mipira mizuri
ya kufunga,”alisema Tambwe ambaye habari za ndani zinadai kwamba baadhi
ya vigogo wa Kundi la Friends of Simba wanajipanga kumtumia kama chambo
kwenye kampeni za uchaguzi wa Simba mwezi ujao.
Mchezaji huyo ana mkataba wa miaka miwili na Simba, lakini
wamekubaliana msimu wa kwanza ukimaliza watakaa chini kujadiliana jinsi
ya kuendelea na mwaka wa pili.
Habari zinadai kwamba vigogo hao wamepanga kumlipa fedha za mkataba
wa mwaka wa pili na kumhakikishia maisha mazuri Simba na watatumia
upenyo huo kama sehemu ya kampeni za uchaguzi wa mwezi ujao.
SOURCE: MWANASPOTI