Na Karoli Vinsent -- MAMLAKA ya Mawasiliano nchini (TCRA) imevipa onyo
kali vituo vya habari vya ITV na Star Tv pamoja na Radio Free Africa,
kwa kurusha tangazo lililoelezwa kuwa ni kinyume na maadili.
Onyo hilo limetolewa leo Jijini Dar es Salaam katika mkutano na Waandishi wa Habari na Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka hiyo, Margaret Mnyagi ambaye alisema Kamati imefikia maamuzi hayo baada ya kushauriana na Kamati Maudhui ya vipindi vya runinga vya mamlaka hiyo.
“Tumefika maamuzi haya baada ya kukaa sisi kama kamati ya Maudhui na kubaini tangazo la Policy Forum ambalo tangazo hilo linachochoe watu wasilipekodi,Tangazo hilo lilirushwa kwenye Runinga mbili ambazo ni Itv pamoja na Startv na redio ambayo ni Radio Free”
“Napenda kuwatoa hofu wananchi kuwa atuchafanya upendeleo wowote katika kutoa hukumu hii”
alisema Mnyagi
Aidha Mamlaka hiyo imevitaka vyombo hivyo vilivyorusha Tangazo hilo viwasilishe mwongozo wa urushaji wa matangazo hayo,na pia Mamlaka hiyo imevionya vyombo hivyo kutorudia kuonyesha Matangazo ya uchochezi, na endapo watakaidi Mamlaka hiyo itawachukulia hatua kali za kisheria.
Meneja wa Mipango na Utafiti wa Sahara Media. Nassan Lwehabula ambao ni wamiliki wa Star Tv, Kiss FM, Radio Free Africa na Gazeti la Msanii wa Afrika alisema wao wamechukulia onyo hilo kama changamoto kwao ya kufanya vipindi vyao kwa umakini.
Tangazo liloifanya Mamlaka ya Mawasiliano nchini kuchukua Maamuzi hayo ni Tangazo la Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali inayojulikana kama Policy Forum, ambayo katika tangazo hilo waliwahamasisha wananchi wasilipe kodi katika mwezi wa Januari, mwaka huu.

No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako