Habari
jamani. Ninaandika ujumbe huu kwa kuomba msaada. Mtanzania mwenzetu
amefariki in Madison Wisconsin-USA, wanatafutwa ndugu zake. Ni mtu wa
Tanga Michael Agustine Lukindo. Alikuja
USA miaka mingi iliyopita, inasemekana zaidi ya mika thelathini.
Ameacha
mke (African American) na watoto wanne, mkubwa alizaliwa 1989 familia
yake haijui ndugu za Michael. Mazishi yatafanyika Jumamosi, ila mwili
utachomwa.
Kama unafununu au kujua lolote kuhusiana na ndugu yetu huyu
unijulishe. Lengo nikuweza kuwafahamisha ndugu zake nyumbani Tanzania.
Asante kwa ushirikiano wako.